Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-USALAMA

Jaribio la mapinduzi nchini Guinea-Bissau: "Hali imedhibitiwa", asema Rais Embalo

"Hali imedhibitiwa," Rais Embalo ameambia waanishi wa habari siku ya Jumanne jioni, baada ya sintofahamu kuripotiwa Jumanne hii, Februari 1, 2022, mjini Bissau. Milio ya risasi ilisikika katikati mwa mji huo karibu na taasisi za nchi. Milipuko iliyosababisha wakazi kupatwa na hofu.

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya jaribio la mapinduzi lililotokea Februari 1, 2022.
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya jaribio la mapinduzi lililotokea Februari 1, 2022. © AFP/AFPTV/Aliu Embalo
Matangazo ya kibiashara

Rais Embalo alionekana mbele ya waandishi wa habari Jumanne jioni baada ya masaa kadhaa ya sintofahamu katika mji mkuu wa Guinea-Bissau. Akiwa amezungukwa na Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria, Umaro Sissoco Embalo alivishukuru vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kwa kuzuia mapinduzi hayo ambayo lengo ilikuwa ni "kuhatarisha demokrasia".

“Kilikuwa ni kitendo kilichoandaliwa na kupangwa”, amesema rais wa Guinea-Bissau, ambaye alihusisha jaribio hili la mapinduzi na “maamuzi (aliyoyachukua), hususan mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na ufisadi”, bila kuwataja wazi wahusika wa mapinduzi hayo . "Washambuliaji waliweza kuzungumza nami kabla ya matukio haya ya umwagaji damu ambayo yasababisha vifo vya watu kadhaa na wengine kujeruhiwa vibaya", alisikitika Rais Umaro Sissoco Embalo, bila hata hivyo kutaja idadi ya watu waliouawa.

Kiongozi huyo amedai kulikuwa na mpango wa kumuua yeye na Baraza lake la Mawaziri na watu waliojihami kwa kile anachosema ni kutokana na juhudi zake za kupambana na ufisadi na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress, amelaani kilichotokea nchini Guinea Bissau na kutaka taasisi ya kidemokrasia kuheshimiwa.

Umoja wa Afrika na Jumuiya ya ECOWAS inayoleta pamoja nchi za Afrika Magharibi, imeshtumu pia jaribio hilo la mapinduzi . Kwa sasa hali inaelezwa kuwa tulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.