Pata taarifa kuu

Jeshi ladai kuzima jaribio la mapinduzi Guinea-Bissau

Mkuu wa majeshi nchini Guinea-Bissau ametangaza kwamba jeshi limezuia na kuzima jaribio la mapinduzi lililokuwa likiandaliwa na kundi la watu.

Mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau.
Mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau. © Charlotte Idrac / RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika hafla ya sherehe ya kuadhimisha miaka 47 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi nchini Guinea-Bissau, Jenerali Biagué Na Ntan alitangaza kwamba "kundi la wanajeshi wa FARP (Vikosi vya Wanajeshi vya Mapinduzi)" wanaohusikakatika maandalizi ya jaribio hilo limetambuliwa.

Kulingana na kauli yake, kundi hili lilikuwa "likihamasisha wanajeshi baada ya kupewa fedha ili kupotosha utaratibu uliowekwa wa kikatiba".

Tangazo hilo linalokuja wakati rais Umaru Sissoco Embalo yuko ziarani nchini Ufaransa. Atapokelewa leo Ijumaa asubuhi katika Ikulu ya Élysée na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.