Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-USALAMA

Guinea-Bissau: Milio ya risasi yasikika karibu na makao makuu serikali

Sintofahamu imerpotiwa Jumanne hii, Februari 1, 2022, mjini Bissau, mji mkuu wa Guinea-Bissau. Milio ya risasi imesikika katikati mwa jiji karibu na taasisi za nchi. Milipuko iliyosababisha wakaazi wa mji huo kuwa na hofu. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Mgharibi, ECOWAS,  inalaani "jaribio la mapinduzi. "

Makao makuu ya Serikali nchini Guinea-Bissau.
Makao makuu ya Serikali nchini Guinea-Bissau. © LUSA
Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi imesikika mapema mchana karibu na makao makuu ya serikali, wakati kikao cha Baraza la Mawaziri kilikuwa kikifanyika. Rais wa Jamhuri, Umaro Sissoco Embalo, Waziri Mkuu Nuno Gomes Nabiam na wajumbe wengine wa serikali walikuwa wakisiriki mkutano huo. Kikao kilikatizwa.

Tangu habari hizo kuenea, kumekuwa na mkanyagano katikati ya jiji la Bissau. Shule zimefungwa na watoto wamerudi nyumbani.

Wanajeshi wengi wameonekana katika mji mkuu wa Guinea-Bissau. Vikosi vya wanajeshi waliojihami kwa silaha za kivita wametumwa karibu na baadhi ya majengo ya serikali. Kwa sasa, haijulikani nia ya washambuliaji wala hatima ya Rais Embalo.

Shirika la habari la Ureno Lusa linaripoti takriban majeruhi wanne, akiwemo mmoja aliye katika hali mbaya, likinukuu chanzo kutoka Hospitali ya Simão Mendes huko Bissau.

ECOWAS yalaani "jaribio la mapinduzi"

Katika taarifa iliyotolewa saa chache baada ya tukio hilo, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi "imelaani jaribio hili la mapinduzi na imewatka wanajeshi kutomfanyia chochote kibaya Rais Umaro Sissoco Embalo na wajumbe wa serikali yake".

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa "kukomeshwa mara moja" kwa "mapigano makali" huko Bissau na "kuhesimu taasisi za nchi zilizochaguliwa kidemokrasia", imesema taarifa hiyo.

Matukio ambayo yanatokea baada ya kufanyika mabadiliko katika serikali

Matukio haya yanakuja siku chache baada ya mabadiliko ya serikali yaliyoamuliwa na Rais wa Jamhuri Umaro Sissoco Embaló, ambayo hapo awali yalipingwa na chama cha Waziri Mkuu Nuno Gomes Nabiam. Baadaye, hata hivyo, Waziri Mkuu alisema anaunga mkono mabadiliko hayo.

Mahusiano kati ya Rais wa Jamhuri na serikali katika miezi ya hivi karibuni yaligubikwa na hali ya mvutano ambayo ilichochewa zaidi na ndege ya Airbus A340 iliyotua Bissau Oktoba mwaka jana kutoka Gambia kwa idhini ya ofisi ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.