Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Ghana: ECOWAS kuijadili Burkina Faso baada ya mapinduzi

Mkutano usio kuwa wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, unafunguliwa Alhamisi hii asubuhi mjini Accra, mji mkuu wa Ghana.

Rais wa tume ya ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou (kulia) baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya wajumbe kutoka jumuiya hiyo ndogo ya kikanda huko Ougagadougou baada ya mapinduzi nchini Burkina Faso, Januari 31, 2022.
Rais wa tume ya ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou (kulia) baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya wajumbe kutoka jumuiya hiyo ndogo ya kikanda huko Ougagadougou baada ya mapinduzi nchini Burkina Faso, Januari 31, 2022. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Kama bendera za nchi kumi na tano wanachama wa jumuiya hiyo ndogo ya kikanda zitaonekana katika ukumbi wa mkutano, viti vitatu vitasalia tupu: Mali, Guinea na Burkina Faso. Nchi tatu zilizosimamishwa uanachama katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, baada ya mapinduzi ya kijeshi. Na faili la Burkina Faso litakuwa kipaumbele cha Wakuu wa Nchi kutoka jumuiya hiyo.

Viongozi Kadhaa kutoka jumuiya ya ECOWAS, akiwemo raia wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara tayari wametangaza kuwa watashiriki mkutano huo. Baada ya hotuba ya ufunguzi ya Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, kikao cha faragha kitaanza. Ripoti ya ujumbe wa ECOWAS nchini Burkina Faso itasikilizwa kwa umakini na wakuu wa nchi.

Lakini tayari wanadiplomasia hawafichi.  Luteni kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba aliyeongoza mapinduzi nchini Burkina Faso aliweza kujirekebisha kuwa wale waliokutana naye. Kiongozi huyu ambaye alihudumu mwaka mzima nchini Mali kutoka mwaka 2020 hadi mwaka wa 2021 kama "Mlinda amani" wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha Minusma. Alirejesha Katiba ya nchi yake baada ya kuisimamisha mara tu mapinduzi yalipotangazwa.

"Nchini Burkina, kila kitu kitakwenda sambamba na kipindi wa mpito. Inabidi kuwepo na kipindi kifupi cha mpito, "amebaini afisa anayefahamu sana jambo hilo. Katika mkutano huo, hali nchini Mali na Guinea - nchi nyingine mbili zinazotawaliwa na kundi la wanjshi waliofanya mapinduzi - zitajadiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.