Pata taarifa kuu

Ouattara kusaidia Burkina Faso katika mapambano yake dhidi ya ugaidi

Tangu Jumamosi Januari 29, sauti ya Alassane Ouattara iliorekodiwa wakati wa mkutano wa mwisho wa wakuu wa nchi za ECOWAS ulioitishwa siku ya Ijumaa baada ya mzozo nchini Burkina Faso inasambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara.
Rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara. John MacDougall/Pool via REUTERS/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Côte d'Ivoire anasikika akielezea msimamo wa nchi yake kuhusu matukio haya na mahojiano yake ya simu na Roch Kaboré, siku ya kupinduliwa kwake.

Hata hivyo, Alassane Ouattara anasikika katika sauti hiyo ya dakika zaidi ya 7, akihutubia mkutano wa wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, siku ya Ijumaa na kuelezea msimamo wa Côte d'Ivoire.

Baada ya kulaani mapinduzi dhidi ya rais Kaboré na kutaka aachiliwe mara moja, rais wa Côte d'Ivoire alitoa vipaumbele vyake viwili: "kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba na kuisdaia Burkina Faso katika mapambano dhidi ya ugaidi ili kuepusha kuanguka kabisa kwa nchi hiyo, hali ambayo inaweza kuwa tishio kwa amani na usalama wa ukanda wetu. »

Taarifa ya mwisho haijataja msaada wa kijeshi mara moja, lakini ECOWAS ilituma ujumbe wa wakuu wa majeshi siku iliyofuata kutathmini hali, hasa usalama.

Katika sauti hii, Alassane Ouattara pia anasimulia mazungumzo ya simu aliyokuwa nayo na Roch Kaboré "Jumatatu alasiri". Roch Kaboré alimfahamisha kuhusu nia yake ya kujiuzulu, jambo ambalo rais wa Côte d'Ivoire alijaribu kumzuia ili kuwapa muda wakuu wa nchi za ukanda huo.

"Aliona kuwa kujiuzulu kwake ndilo jambo pekee la kufanya, kwa sababu hakuingia katika siasa ili kufanya mauaji miongoni mwa wananchi wake," anasema Alassane Ouattara.

Katika sauti hii, pia Alassane Ouattara anasikika akizungumzia hali nchini Mali. Anaomba kufunguliwa kwa majadiliano na serikali ya mpito ili kuandaa "ratiba ya kuaminika ambayo inaweza kuwasilishwa kwa ECOWAS ili iweze kujadiliwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.