Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso yatangaza kurejesha Katiba, jeshi lapewa mamlaka makubwa

Uongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso umetangaza kurejesha katiba na kumtaja kiongozi wa mapinduzi Luteni Kanali Henri Sandaogo Damiba kuwa rais wa mpito. Hatua hii imekuja wiki moja baada ya kutwaa mamlaka katika nchi hii ya ukanda wa Sahel

Luteni Kanali Cyprien Kaboré, wakati wa hotuba alioitoa kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso, Januari 31, 2022.
Luteni Kanali Cyprien Kaboré, wakati wa hotuba alioitoa kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso, Januari 31, 2022. © RTB/Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Kanali Cyprien Kaboré msemaji wa serikali ya kijeshi ndiye aliyesoma uamuzi huo kupitia Televisheni ya taifa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Afrika Magharibi Saleh Annadif, amesema mazungumzo kati yake, wajumbe wa ECOWAS na uongozi wa kijeshi yamekuwa ya wazi.

Juhudi hizo za mazungumzo zinakuja muda mfupi baada ya Umoja wa Afrika kusimamisha uanachama wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi ya Januari 24. ECOWAS nayo ilisimamisha uanachama wa taifa hilo tangu siku ya Ijumaa na kuonya juu ya uwezekano wa vikwazo kulingana na matokeo ya mazungumzo na viongozi wa kijeshi.

Viongozi wa jumuiya hiyo watafanya mkutano wa kilele mjini Accra Ghana siku ya Alhamis, ili kutathmini matokeo ya mazungumzo na viongozi wa jeshi na kuamua ikiwa watatangaza vikwazo dhidi ya Burkina Faso. Katika kipindi cha nyuma ECOWAS ilisimamisha na kutangaza vikwazo dhidi ya wanachama wake wawili Mali na Guinea ambazo zote zimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi ndani ya miezi 18 iliyopita.

Rais aliyeondolewa madarakani Roch Marc Christian Kabore bado yuko kizuizi cha nyumbani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.