Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Wajumbe wa ECOWAS na Umoja wa Mataifa wakutana na rais Kaboré

Ujumbe wa pamoja wa ECOWAS na Umoja wa Mataifa ulikuwa mjini Ouagadougou Jumatatu, Januari 31, kwa mazungumzo na viongozi wa mapinduzi, madarakani kwa wiki moja sasa nchini Burkina Faso. Ujumbe huo pia uliweza kukutana kwa mazungumzo na Rais aliyeondolewa madarakani Roch Marc Christian Kaboré, ambaye anazuiliwa na jeshi.

Shirley Ayorkor Botchway, mkuu wa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini Burkina Faso, na rais wa Kamisheni ya ECOWAS Jean-Claude Brou wakizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wao na rais aliyeondolewa madarakani Roch Kaboré na kiongozi mpya wa kijeshi wa Burkina Faso, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Januari 31, 2022.
Shirley Ayorkor Botchway, mkuu wa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini Burkina Faso, na rais wa Kamisheni ya ECOWAS Jean-Claude Brou wakizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wao na rais aliyeondolewa madarakani Roch Kaboré na kiongozi mpya wa kijeshi wa Burkina Faso, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Januari 31, 2022. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Hili lilikuwa moja ya ombi la ujumbe wa pamoja, unaoundwa hasa na mawaziri wanne kutoka nchi za Afrika Magharibi na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi na Sahel, Mahamat Saleh Annadif: kukutana na rais Roch Marc Christian Kaboré, aliyepinduliwa madarakani Jumatatu iliyopita na bado anashikiliwa. viongiozi wa mapinduzi.

"Bw. Kaboré yuko katika hali nzuri. Yko sawa kiafya. Na anaonana na madaktari wake. Ndivyo alivyotuambia yeye mwenyewe. Na anaruhusiwa kutembelewa na familia yake. ", amesema Waziri wa Mmbo ya Nje wa Ghana Shirley Botchway, kabla ya kuondoka Burkina Faso. Wajumbe hao pia walirejelea matakwa ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nnchi za Aafrika Magharibi, ECOWAS, ya kuona rais wa zamani wa Burkina Fso akiachiliwa haraka.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ghana ambaye anaongoza ujumbe wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS Shirley Ayorkor Botchway, amesema mazungumzo ya mjini Ouagadougou na viongozi wa kijeshi "yalikuwa ya kweli" na kwamba viongozi wa kijeshi walionekana kuyapokea mapendekezo yaliyotolewa, akiitaja kuwa ishara nzuri.

Kabla ya hapo, wajumbe hao walikutana kwa karibu saa tatu na wajumbe wa mamlaka mpya, akiwemo rais wa Vuguvugu la Wazalendo la MPSR, Luteni Kanali Damiba.

"Tulijadili njia na uwezo wa kutoka katika mgogoro huo na kwa kiwango gani jumuiya ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na ECOWAS wanaweza kuwaunga mkono na tulipatabaadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa tayari", amesema Mahamat Saleh Annadif ambaye ameeleza kuwa mazungumzo yao yalikuwa ya "wazi ."

"Nadhani tulielewana vizuri kwa mkutano wa kwanza. Pia kulikuwa na mazungumzo mazuri sana na Mkuu wa Nchi, " amesema Jean-Claude Brou.

Viongozi wa jumuiya hiyo watafanya mkutano wa kilele mjini Accra Ghana siku ya Alhamisi, ili kutathmini matokeo ya mazungumzo na viongozi wa jeshi na kuamua ikiwa watatangaza vikwazo dhidi ya Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.