Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Rais wa zamani Alpha Condé sasa anaishi katika nyumba ya familia

Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano na Maendeleo, CNRD inayotawala Guinea, "itaendelea kuhakikisha mkuu wa zamani wa nchi anahudumiwa kulingana na cheo chake, na hii bila shinikizo lolote. kitaifa na kimataifa, " imesema taarifa hiyo ya kamati hiyo.

Aliye kuwa rais wa Guinea Alpha Condé.
Aliye kuwa rais wa Guinea Alpha Condé. WU HONG / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuachiliwa kwa Bw. Condé ni sehemu ya matakwa ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi sita. ECOWAS iliisimamisha Guinea kataka taasisi zake na kuwawekea vikwazo viongozi wa mapinduzi.

Kiongozi mkuu wa mapinduzi, Kanali Mamady Doumbouya, ambaye alitawadhwa kuwa rais wa mpito Oktoba 1, aliahidi kurejesha mamlaka kwa raia baada ya uchaguzi, lakini hadi sasa amekataa makataa yoyote kuhusiana na kipindi cha mpito.

Katika mahojiano yaliyorushwa na televisheni ya taifa katikati ya mwezi wa Novemba, alihakikisha kwamba uadilifu Bw. Condé analindwa, lakini haijakataza Bw. Condé kuhukumiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.