Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Alpha Condé aruhusiwa kwenda nje kufanyiwa matibabu

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Condé sasa anaweza kuondoka nchini mwake na kuweza kushauriana na madaktari wake nje ya nchi, kwa sharti tu safari hii isizidi mwezi mmoja, labda madaktari waamuwe vinginevyo.

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Condé, Agosti 6, 2020.
Rais wa zamani wa Guinea Alpha Condé, Agosti 6, 2020. CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wapya wa Conakry wamekubali ombi kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya ECOWAS ambao walituma barua kwa Kanali Mamadi Doumbouya Desemba 23, 2021.

Ilikuwa ni baada ya kuzingatia ahadi ya ECOWAS inayohusiana na uwezekano wa Alpha Condé kwenda nje ya nchi kwa uchunguzi wa kimatibabu ambao muda wake hauwezi kuzidi mwezi mmoja ndipo mamlaka ya Guinea imeamua kuweza ufanya safari hiyo kumwachilia katika siku chache zijazo.

Hatua hiyo imepongezwa na wafuasi wa rais huyo wa zamani ambao wanatarajia hatua zaidi za ka manufaa ya kiongozi wao. Souleymane Keita, mbunge wa zamani na msemaji wa chama cha RPG amesema: “Tulipokea taarifa hii kwa furaha kubwa. Kufikia Septemba 5, hatuna taarifa kutoka kwa rais. Wasiwasi wetu kuu ulikuwa kuhusu afya yake. Kwakweli hatua hii imetupa faraja kubwa katika chama cha RPG na wafuasi wetu wote. Tunatumahi kuwa katika siku za usoni atakuwa na fursa ya kupata tena uhuru wake kama tulivyokuwa tukitamani ”.

Mashirika ya kiraia pia yanakaribisha hatua hii ya kibinadamu, lakini wakati huo huo yamesema kushangazwa. Bailo Barry kutoka shirika lisilo la kiseikali la Destin en main anasema: "Ndiyo, ana haki ya kupewa matibabu. Lakini, alindwe, awekwe kwenye eneo la usalama kila wakati ili asiwezi kuwasiliana wanasiasa wanaomuunga mkono ".

Alpha Condé, ambaye aliingia madarakani Desemba 2010, alirejea madarakani mwaka wa 2015 kabla ya kuwania muhula wa tatu jambo ambalo lilipelekea kuanguka kwa utawala wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.