Pata taarifa kuu
GUINEA-HAKI

Conde kukabiliwa na mashitaka kuhusiana na makosa ya jinai wakati wa utawala wake

Nchini Guinea, vyombo vya kisheria, vimeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya aliyekuwa rais Alpha Conde aliyeondolewa na jeshi mwezi Septemba mwaka uliopita, kushiriki kwenye makosa ya jinai wakati akiwa madarakani kati ya mwaka 2010 mpaka 2020.

Kuachiliwa kwa Bw. Condé ni sehemu ya matakwa ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Kuachiliwa kwa Bw. Condé ni sehemu ya matakwa ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). AP - Pablo Martinez Monsivais
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mashtaka Alphonse Charles Wright amesema baadae mashahidi wataitwa kuandikisha na kutoa ushahidi wao katika kipindi hicho cha uchunguzi.

Conde mwenye umri wa miaka 83, aliyekuwa amepewa kifungo cha nyumbani aliruhusiwa kwenda nje ya nchi kupewa matibabu.

Kuachiliwa kwa Bw. Condé ni sehemu ya matakwa ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi sita. ECOWAS iliisimamisha Guinea kataka taasisi zake na kuwawekea vikwazo viongozi wa mapinduzi.

Kiongozi mkuu wa mapinduzi, Kanali Mamady Doumbouya, ambaye alitawadhwa kuwa rais wa mpito Oktoba 1, aliahidi kurejesha mamlaka kwa raia baada ya uchaguzi, lakini hadi sasa amekataa makataa yoyote kuhusiana na kipindi cha mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.