Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Serikali ya Mali kuandamana dhidi ya vikwazo vya ECOWAS

Serikali ya Mali inayotawaliwa na jeshi, imeitisha maandamano ya nchi nzima siku ya Ijumaa, kuendelea kulaani vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Rais wa Mali Assimi Goita.
Rais wa Mali Assimi Goita. AFP - NIPAH DENNIS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Mali, Kanali Asimi Goita amesema, vikwazo hivyo ambavyo ni pamoja na nchi yake kufungiwa mipaka na kuzuiwa kuifanya biashara, vinawatesa wananchi.

Aidha, amesema, atakuja na mpango wa kuhakikisha kuwa, uhuru wa nchi yake unalindwa baada ya kuwekewa vikwazo.

Hatua hii ya ECOWAS ilichukuliwa Jumapili iliyopita, baada ya kudhihirika kuwa, serikali ya Mali ambayo ni ya mpito, haina mpango wa kuandaa uchaguzi kufikia mwezi Februari kama ilivyopangwa na badala yake inataka uchaguzi huo ufanyike baada ya miaka mitano.

Mbali na ECOWAS, vikwazo hivyo vimeungwa mkono na Ufaransa ambayo ilikuwa koloni ya nchi hiyo, lakini pia na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Serikali ya Mali, imekuwa ikisema changamoto za kiusalama ndio sababu kubwa inayosababisha ishindwe kuandaa uchaguzi salama ifikapo mwisho wa mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.