Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali yajibu baada ya ECOWAS kutangaza vikwazo dhidi yake

Serikali ya mpito nchini Mali inayoongozwa na jeshi, imelaani hatua ya nchi za Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS, kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na diplomasia, kufuatia uamuzi wa serikali hiyo kuendelea kuwa madarakani mpaka 2025.

Assimi Goita, Rais wa mpito wa Mali. Juni 7, 2021.
Assimi Goita, Rais wa mpito wa Mali. Juni 7, 2021. AFP - ANNIE RISEMBERG
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali hiyo Kanali, Abdoulaye Maiga amesema vikwazo hivyo ni kinyume cha sheria na kufuatia hatua hiyo, imefunga mipaka yake ya ardhini na angani na kuwataka mabalozi wake kwenye nchi za Afrika Magharibi kurejea jijini Bamako

Uamuzi wa kuiwekea vikwazo Mali ulifanywa na viongozi hao waliokutana jijini Accra siku ya Jumapili, ikiwa ni mwendelezo wa kuishinikiza Mali kuandaa uchaguzi mwezi Februari.

Hata hivyo, kamati maalum iliyoteuliwa na uongozi wa Mali ulishauri kuwa uchaguzi utafanyika baada ya miaka mitano kwa sababu za kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.