Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Vikwazo vya ECOWAS: Hali isiyowezekana kwa uchumi wa Mali

Vikwazo vya kiuchumi na kifedha vilivyopitishwa na viongozi wa ECOWAS ni vizito sana kwa Mali. Kufungiwa kwa mali ya Mali, kusimamishwa kwa shughuli za kibiashara na Bamako na kufungwa kwa mipaka kwa kweli kunasababisha wasiwasi mkubwa nchini Mali.

Makao makuu ya Benki Kuu ya Afrika Magharibi (BCEAO) huko Bamako, Mali.
Makao makuu ya Benki Kuu ya Afrika Magharibi (BCEAO) huko Bamako, Mali. © AFP - Annie Risemberg
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi havivumiliki. Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Mgharibi, ECOWAS, imeweka uchumi wa Mali katika hali isiyowezekana. Nchi haina tena uwezo wa kufikia akaunti zake zilizoko benki ya BCEAO, benki kuu katika ukanda huo. Ni kana kwamba mtu binafsi hawezi kufikia tena akaunti yake ya benki au kutumia kadi ya kielektroniki ya kutoa pesa kwenye akaunti yake ya benki. Kwa hiyo anaweza tu kutumia kile alichonacho mfukoni mwake. Nchi ya Mali itaweza tu kutumia kile ambacho imeweka kando katika hazina ya umma.

"Kwa kweli, inadhoofisha uchumi wa Mali. Na kuna uwezekano mkubwa kwamba baada ya mwezi mmoja au miwili hatutaweza hata kulipa mishahara ya watumishi wetu wa umma. Kwa vyovyote vile, hakutakuwa na uingizwaji wa pesa kutoka benki ya BCEAO katika uchumi wa Mali. Kwa hivyo tutafanya kazi kimsingi na ukwasi katika mzunguko na amana katika kiwango cha benki zingine ndogo ndogo, "amebaini Etienne Fakaba Sissoko, profesa wa uchumi na mtafiti katika Kituo cha Uchambuzi wa Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.