Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Waziri mkuu Abdalla Hamdok ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok ametangaza kujiuzulu, wiki chache tu baada ya kurejeshwa kwenye nafasi hiyo na uongozi wa jeshi uliochukua madaraka mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok aliyjiuzulu Novemba 21, 2021 mjini Khartoum alikaporejeshwa madarakani na jeshi.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok aliyjiuzulu Novemba 21, 2021 mjini Khartoum alikaporejeshwa madarakani na jeshi. Ebrahim HAMID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Hamdok inakuja kufuatia maandamano ya wiki kadhaa ambayo yamekuwa yakiendelea jijini Khartoum na miji mingine, kupinga mkataba wa kisiasa uliofikiwa kati yake na jeshi.

Waandamanaji wakiongizwa na vuguvugu la kiraia, wamekuwa wakisema wanataka, uongozi wa kiraia na sio wa kijeshi chini ya Abdel Fattah al-Burhan.

Kupitia Televisheni ya taifa, Hamdok ameelezea sababu za kujiuzulu kwake.

Nimeamua kuatangza kujizulu, kutoa nafasi kwa mtu mwingine mwanaume au mwanamke kuendelea na kazi katika taifa letu, zuri, nimejaribu kwa uwezo wangu wote kuhakikisha kuwa nchi yetu hairudi kwenye mizozo, lakini nchi yetu ilikofika, ipo kwenye hatari kubwa ya kutumbukia kwenye mzozo mkubwa unaitishia uhai wake.

Kabla ya kuchukua hatua hiyo, kulikuwa na maandamano jijini Khartoum siku ya Jumapili na kusababisha makabiliano makali kati ya maafisa wa usalama na polisi, na madaktari wanasema watu wawili wamepoteza maisha na kufikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia zaidi ya Hamsini tangu kuanza kwa maandamano hayo mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Kujiuzulu kwa Hamdok, kunaicha Sudan kwenye mzozo mwingine wa kisiasa, katika taifa ambalo limeendelea kuwa na historia ya mapinduzi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.