Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Sudan: Wawili wauawa katika maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi

Sudan imeendelea kukumbwa na maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi. Waandamanaji wamerudi kwa maelfu mitaani "kwa kuwakumbuka mashujaa". Lakini wawili kati yao wamepoteza katika maandamano hayo, kulinana na mashahidi, na kufanya jumla ya watu 56 waliouawa na mamia kujeruhiwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Jenerali Abdel Fattah al- Burhane, tarehe 25 Oktoba.

Wanawake wa Sudan wakiandamana kupinga mapinduzi katika mitaa ya Khartoum, Novemba 17, 2021.
Wanawake wa Sudan wakiandamana kupinga mapinduzi katika mitaa ya Khartoum, Novemba 17, 2021. © AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Mji mkuu wa Sudan umezingirwa na wanajeshi. Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi waliokusanyika kwenye ikulu ya rais.

Tangu asubuhi sana, vikosi vya usalama vimefunga madaraja yanayounganisha mji wa Khartoum na vitongoji vyake. Kwenye barabara kuu za mji mkuu, magari ya kivita yaliyo na bunduki nzito yalitumwa, kama kila Jumapili ya maandamano.

Wawili wamepoteza maisha katika viunga vya Khartoum

Huko Omdourman, kitongoji cha kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, kumeripotiwa vifo vya watu wengine wawili. Mmoja wao amepigwa risasi kifuani, kwa mujibu wa muungano wa madaktari wanaounga mkono demokrasia. Mtu wa pili "amepigwa vikali kichwani hadi fuvu la kichwa kuvunjika", kulingana na madaktari hao.

Vikosi vya usalama vya Sudan mara kwa mara huwapiga waandamanaji kwa fimbo. Na tangu mapinduzi ya Oktoba 25, jumla ya waandamanaji 56 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa. Alhamisi iliyopita, waandamanaji watano waliuawa kwa kupigwa risasi mjini Khartoum, kulingana na muungano wa madaktari hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.