Pata taarifa kuu

WFP yasitisha shughuli zake baada ya visa vya uporaji katika jimbo la Darfur

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limelazimika kusitisha shughuli zake katika jimbo la Darfur Kaskazini, nchini Sudan, kutokana na visa vya uporaji vilivyoripotiwa kuanzia Jumanne hadi Alhamisi, katika maghala yake, vitendo vilivyofanywa na watu wenye silaha huko El-Fasher. Kwa jumla, zaidi ya tani 5,000 za chakula na vifaa vyote viliibiwa.

Katika soko kuu la El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini.
Katika soko kuu la El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini. © Sébastien Németh/RFI
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu milioni mbili watalazimika kwenda kokosa msaada wa WFP katika eneo hili la Sudan Kaskazini mwa jimbo la Darfur ambalo linakabiliwa na mzozo mkubwa wa chakula na machafuko mapya.

"Hakuna kilichbaki katika maghala hayo," anasikitika Marianne Ward, kaimu mkurugenzi wa Mpango wa Sudan, akihojiwa na François Mazet wa kitengo cha RFI Kkatika kanda ya Afrika.

"Mtu mmoja kati ya watatu katika Darfur Kaskazini yuko katika hatari ya njaa kali. Hawa ni watu ambao hawawezi kulisha familia zao na hatutaweza kuwasaidia katika kipindi chote cha mwezi wa Januari kwa sababu hatuna chakula huko El-Fasher na pia hatuna vifaa.

Kila kitu kiliibiwa, si chakula tu bali pia hema zetu za kuhifadhia walio na matatizo. Walibomoa kifaa chetu chote cha ugavi. Hakuna kilichosalia isipokuwa vumbi na takataka.

Hatujui ni nani aliyefanya hivi. Mwenendo wa matukio hauko wazi kwetu. Kilicho hakika ni kwamba hali katika eneo hilo imekuwa ngumu kwa muda. Bila usalama hatuwezi kufanya kazi na jamii kwa ujumla haiwezi kufanya kazi. Kitu kingine tunachoomba mamlaka itusaidie kutafuta baadhi ya akiba ya chakula chetu kwa sababu kitauzwa, hivyo tunaomba msaada wao katika kuurejesha,” ameongeza.

Marianne Ward anatumai kuwa baada ya tathmini ya vifaa, WFP inaweza kuanza tena shughuli zake mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.