Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Gambia: Uwepo wa ujumbe wa ECOWAS wazua kizaaza

Nchini Gambia, Rais Adama Barrow, aliyechaguliwa tena katika uchaguzi wa urais mnamo Desemba 4, anatarajiwa kutawazwa Januari 19, miaka mitano baada ya Yayah Jammeh kwenda uhamishoni nchini Equatorial Guinea.

Wanajeshi wa ECOMIG nchini Gambia. Ujumbe huu ulianzishwa baada ya mkwamo wa kisiasa mwaka wa 2017 na kukataa kwa Yahya Jammeh kuachia madaraka.
Wanajeshi wa ECOMIG nchini Gambia. Ujumbe huu ulianzishwa baada ya mkwamo wa kisiasa mwaka wa 2017 na kukataa kwa Yahya Jammeh kuachia madaraka. CARL DE SOUZA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani, ambaye alikuwa ameongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 22, alishinikizwa kuondoka nchini humo ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, kuingilia kati mwezi Januari 2017. Tangu wakati huo, idadi wanajeshi wa jumuiya hiyo imepunguzwa, lakini ujumbe wa ECOMIG, ujumbe wa wa ECOWAS nchini Gambia - bado upo, kwa ombi la mamlaka. Jambo ambalo lilipitishwa sio kwa kauli moja.

Kikosi cha ECOWAS ambacho kinaendelea kuongezewa muda kila mara baada ya muhula wake kumalizika, bado kinatuma takriban wanajeshi elfu moja nchini Gambia, wakiwemo kikosi cha wanajeshi 625 wa Senegal. Lengo la awali lilikuwa ni kuhakikisha utulivu wa nchi hiyo na usalama wa taasisi wakati wa kipindi cha mpito. Kwa upande wa Lamin Barrow, mfuasi wa rais aliyechaguliwa tena, uwepo wa ECOMIG unatia moyo: "Ni jambo zuri kwamba wanajeshi wa ECOWAS bado wako, kwa usalama wetu. "

Lakini miaka mitano baadaye, uwepo wa jeshi hilo hauna maana tena, amesema mfuasi mmoja wa upinzani: "Nadhani ni wakati muafaka wa askari hawa kuondoka. Gambia ni nchi yenye amani. Je, wanasubiri nini? Katika miaka ya hivi karibuni, hakukuwa na matatizo ya usalama. Sielewi kwanini bado wapo. "

Kwa upande wa Ernest Baï Koroma, rais wa zamani wa Sierra Leone na mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa ECOWAS wakati wa uchaguzi wa urais mwezi uliopita, amesema, ni jambo ambalo halitaki  haraka. "Ni juu ya kuhakikisha kuwa zoezi la kuwaondoa askari hao linashughulikiwa vyema," amesema. Kumekuwa na mifano katika nchi nyingine ambapo kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni kumeenda sambamba na kuzorota kwa usalama. Inapaswa kuwa mchakato, ili kuepuka hatari. "

Kikosi cha ECOMIG kipo "kutuunga mkono", "bila malipo", "kwa ajili ya mageuzi ya sekta ya usalama," Adama Barrow alisema baada ya kutangazwa alipochaguliwa tena.

Wakati wa kikao chake mwezi Juni 2021, mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa ECOWAS ulithibitisha uamuzi wake wa "kubadilisha muundo wa ECOMIG" baada ya uchaguzi wa rais wa Gambia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.