Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Wafuasi wa rais Adama Barrow wamiminika mitaani kwa furaha ya ushindi wao

Nchini Gambia, wafuasi wa rais Adama Barrow wamekuwa wakisherehekea ushindi wa mgombea wao, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa urais wa kihistoria uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais aliyechaguliwa tena wa Gambia Adama Barrow akipungia mkono umati wa watu baada ya kushinda uchaguzi wa Disemba 5 mjini Banjul.
Rais aliyechaguliwa tena wa Gambia Adama Barrow akipungia mkono umati wa watu baada ya kushinda uchaguzi wa Disemba 5 mjini Banjul. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi nchini humo ilimtangaza rais Barrow mshindi baada ya kuwashinda wagombea wenzake watano kwa kupata asilimia 53 ya kura zilizopigwa.

Barrow ambaye ameshinda muhula wa pili, amewahotubia wafuasi wake, na kuahidi kuimarisha maisha ya watu wa Gambia.

Hata hivyo, wapinzani wake, wakionpozwa na Ousainou Darboe aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa asilimia 27.7, ameyakataa matokeo hayo, na kulalamikia wizi wa kura.

Waangalizi wa kimataifa walioshuhudia uchaguzi huo, wanasema zoezi hilo lilikuwa huru na lilifanyika kwa utulivu. Kiongozi wa waangalizi kutoka ECOWAS Ernest Bai Koroma, amewataka raia wa nchi hiyo kukubali matokeo yaliyotangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.