Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO

Sudan: Maelfu ya waandamanaji waingia tena mitaani

Raia wenye hasira wameingia tena mitaani leo Jumapili. Maelfu ya waandamanaji wamemiminika mitaani huko Khartoum na vitongoji vyake, na mamia huko Madani, mji ulioko kilomita 150 kusini mwa mji mkuu.

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi katika mitaa ya Khartoum Jumamosi hii, Disemba 25.
Maelfu ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi katika mitaa ya Khartoum Jumamosi hii, Disemba 25. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka za mpito zinazoongozwa na Jenerali al-Burhan zimekat intaneti na mawasiliano ya simu. Vyombo vinavyotumiwa hadi sasa na waandamanaji kuandaa mikutano yao.

Kwa upande wa waandamanaji, maandamano haya kwa mara nyingine tena ni njia ya kuelezea upinzani wao kwa utawala wa kijeshi wa Jenerali al-Burhan. "Hakuna mazungumzo" na jeshi. "Askari warudi kambini". Hizi ni kauli mbiu za wapiganaji wa vuguvugu la mapinduzi linalodai uhuru.

Siku ya leo imekuwa na mvutano mkubwa. Kwanza, kwa sababu Khartoum imezingirwa na jeshi, kama ishara ya vitisho vya kuwakatisha tamaa waandamanaji. Barabara kuu katikati mwa jiji ambapo makao makuu ya jeshi yapo zimezuiwa. Kama vile madaraja yanayounganisha katikati mwa mji na vitongoji.

Siku ya Ijumaa, gavana wa Khartoum alionya kwamba "kukaribia au kushambulia majengo ya mamlaka ya kimkakati kunaadhibiwa na sheria."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.