Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

Msumbiji: Mashambulio ya wanajihadi yasababisha wimbi jipya la watu kutoroka makazi yao

Nchini Msumbiji, mashambulizi ya wapiganaji wa kijihadi yanaendelea kutumbukiza eneo la kaskazini mwa nchi katika ukosefu wa usalama. Kulingana na msemaji wa serikali, karibu watu 4,000 walilazimika kutoroka vijiji vyao mwezi wa  Desemba 2021 kutokana na mashambulizi hayo.

Makundi ya waasi yalidhibiti uwanja wa ndege wa Mocimboa da Praia kwa mwaka mmoja. Lakini licha ya kutekwa kwa Mocimboa da Praia kutoka mikononi mwa waasi, ghasia hazijapungua. Zaidi ya watu 4,000 walilazimika kutoroka vijiji vyao mwezi Desemba 2021 kwa sababu ya mashambulizi ya waasi.
Makundi ya waasi yalidhibiti uwanja wa ndege wa Mocimboa da Praia kwa mwaka mmoja. Lakini licha ya kutekwa kwa Mocimboa da Praia kutoka mikononi mwa waasi, ghasia hazijapungua. Zaidi ya watu 4,000 walilazimika kutoroka vijiji vyao mwezi Desemba 2021 kwa sababu ya mashambulizi ya waasi. LUSA - LUIS MIGUEL FONSECA
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wa kijihadi wanaendesha mashambulizi katika jimbo la Cabo Delgado kaskazini mashariki mwa Msumbiji kwa miaka minne. Lakini tangu mwisho wa mwezi wa Novemba, mashambulizi yameongezeka nje ya eneo la kawaida la wanajihadi.

Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu jimbo la Niassa, lililoko magharibi mwa Cabo Delgado, pia kulengwa na mashambulizi ya waasi. Wapiganaji walitimuliwa katika eneo lao la kawaida kwa mafanikio ya wanajeshi wa serikali na washirika wao, kulingana na Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi.

Tangu mwezi Julai, zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Afrika Kusini na Rwanda, pamoja na wakufunzi wa Ulaya na Marekani, wamesaidia na kutoa mafunzo kwa jeshi la Msumbiji, ambalo haliwezi kukabiliana na tishio la wanajihadi peke yake.

Kuhama kutokana na vurugu nchini

Licha ya ushindi ulionekana kwenye uwanja wa vita kama vile kutekwa kwa mji wa Mocímboa da Praia, iliyokuwa ngome ya waasi, machafuko yanaendelea. Katika jimbo la Niassa, waliotoroka makazi yao wanakimbia mashambulizi hayo ili kupata hifadhi katika mji wa Mecula.

Mapigano mapya, hapo awali yaliyopuuzwa na mamlaka ambayo iliwataka raia wasiwe na hofu. Lakini leo, kutokana na watu kutoroka makazi yao kutokana na kmachafuko katika jimbo hilo jirani, wataalamu wanataka kuangaliwa upya kwa mapambano dhidi ya wanajihadi nchini humo. Ujumbe wa usaidizi wa SADC, uliopata hasara kubwa baada ya kupoteza wanajeshi wake mwishoni mwa mwezi Desemba, unaweza kuona muda wake ukiongezwa hadi mwezi Januari.

Waasi hawa waligundua kuwa hawawezi kushikilia ngome zao na kwa hivyo walihamia mkoa mwingine. Lakini eneo hili si rahisi kwa uporaji na utekaji nyara waliotumia huko Cabo Delgado.

Alex Vines kutoka shirika la Think tank Chatham House anasema: waasi "wako chini ya shinikizo"

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.