Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

Msumbiji: HRW lashushia lawama jeshi kuwazuia watu wanaohofiwa kushambuliwa

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema wanajeshi wa Msumbiji wanawazuia maelfu ya watu wanaokimbia makwao Kaskazini mwa nchi hiyo kwa kuhofia kushambuliwa kutoka wanajihadi.

Maafisa wa Polisi na askari wa Rwanda kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (FDR) wakielekea Msumbiji katika ujumbe wa kijeshi, katika uwanja wa ndege wa Kanombe, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021.
Maafisa wa Polisi na askari wa Rwanda kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (FDR) wakielekea Msumbiji katika ujumbe wa kijeshi, katika uwanja wa ndege wa Kanombe, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, Jeshi la Rwanda linasema limepiga hatua kubwa kwenye mapambano dhidi ya majihadi katika mkoa wa Cabo Delgado, kulingana na Kanali Ronald Rwivanga, msemaji wa Jeshi la Rwanda linaloshiriki kwenye operesheni dhidi ya Majihadi nchini Msumbiji.

Wanajeshi 1000 wa Rwanda walitumwa nchini Msumbiji kukabiliana na wapiganaji ambao wamefanya mashambulizi ya uharibifu kaskazini mwa taifa hilo.

Katika kipindi cha wiki mbili - kundi la kwanza la wanajeshi wa kigeni kuwasili nchini humo dhidi ya wapiganaji hao , limeteka eneo muhimu lenye barabara ya makutano , ambalo lilikuwa likishikiliwa na wapiganaji hao kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita , na wamefika katika mji muhimu wa Mocimboa da Praia.

Katika kipindi cha miaka minne wapiganaji hao walichukua udhibiti wa wilaya tano muhimu katika mkoa wa Cabo Delgado katika eneo la mashariki la Msumbiji.

Kufikia sasa takriban watu 3,100 wameuawa na wengine 820, 000 kuwachwa bila makao.

Wakati makundi ya uasi yalipoteka mji wa Palma mwezi Machi, mji wenye utajiri wa gesi ambako kunatengenezwa kiwanda chenye thamani ya dola bilioni 20 (£14bn) kikiwa ni kiwanda cha pili kwa ukubwa barani Afrika, Kampuni ya Ufaransa ya mafuta ililazimika kuacha ujenzi mkubwa katika eneo hilo.

Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi, lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.