Pata taarifa kuu
RWANDA-USALAMA

Polisi nchini Rwanda yawakamata washukiwa 13 wa ugaidi

Polisi nchini Rwanda wamewakamata watu 13 wanaoshukiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi jijini Kigali.

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Polisi wamewaonesha washukiwa hao hadharani kwa wanahabari na kusema walikamatwa wakiwa na vifaa vya kutengeza bomu, ikiwemo vilipuzi, nyaya, misumari na simu.

Aidha, polisi nchini humo wanasema uchunguzi wao umebaini kuwa, watu hao walikuwa wanashirikiana na waasi wa ADF, linaloendelea kutekeleza mauaji dhidi ya raia Mashariki mwa DRC.

Ukamataji wa kwanza, ulifanyika mwezi Agosti huku wengine mwezi Septemba na walikamatwa katika jiji kuu Kigali, Nyabihu na Rusizi.

Kati ya mwaka 2010 na 2013, Rwanda ilishuhudia mashambulizi ya guruneti.

Hii inakuja wakati huu Jeshi la Rwanda likiendelea na operesheni dhidi ya kundi la kijihadi nchini Msumbiji na ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutuma wanajeshi wake nchini humo na imefanikiwa kuwarudisha nyuma wapiganaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.