Pata taarifa kuu
RWANDA-USHIRIKIANO

Rwanda yapoteza wanajeshi wanne katika mapigano Cabo Delgado

Kulingana na vyombo vya habari vya Rwanda, wanajeshi wanne wa kikosi cha wanajeshi 1,000 kutoka Rwanda waliokwenda nchini Msumbiji kusaidia vikosi vya serikali katika vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu, wameuawa katika jimbo la Cabo Delgado.

Maafisa wa polisi na askari wa Rwanda kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (RDF) walikwenda msumbiji kusaidi vikosi vya serikali kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021.
Maafisa wa polisi na askari wa Rwanda kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (RDF) walikwenda msumbiji kusaidi vikosi vya serikali kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu, Kigali, Rwanda, Julai 10, 2021. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wengine 14 wamejeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa vyombo vya Rwanda

Ni kwa mara ya kwanza Rwanda kutangaza hasara iliyopata katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu huko Cabo Delgado, nchini Msumbiji.

Hii inatokea wakati siku ya Jumamosi Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenyeji wake wa Msumbiji walikuwa wanawapongeza wanajeshi ambao wamejitoa kupambana na magaidi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na rais wa Msumbiji Filipe Nyusi (rklia) wakivali sare za kijeshi Septemba 24, 2021 huko Pemba katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na rais wa Msumbiji Filipe Nyusi (rklia) wakivali sare za kijeshi Septemba 24, 2021 huko Pemba katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji. © SIMON WOHLFAHRT/AFP

Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi , lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji.

Katika kipindi cha miaka minne wapiganaji hao walichukua udhibiti wa wilaya tano muhimu katika mkoa wa Cabo Delgado katika eneo la mashariki la Msumbiji. Hadi sasa watu 3,100 wameuawa na wengine zaidi ya 820,000 wamekimbia makazi yao -ikiwa ni zaidi ya idadi yote ya watu wa wilaya tano.

Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi, lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji.
Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi, lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji. LUSA - LUIS MIGUEL FONSECA
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.