Pata taarifa kuu

ECOWAS yaandaa mkutano wa kilele wa Novemba 7 ili kuhusu Mali na Guinea

Ndani ya wiki moja tu, wakuu wa nchi za Afrika Magharibi watakutana kwa mkutano wa kilele usio wa kawaida. Hii ni habari ya RFI. Mkutano wa kilele wa ECOWAS kwa umepangwa kufanyika Novemba 7 ili kutoa uamuzi kuhusu maendeleo ya kipindi cha mpito nchini Guinea, ambapo wajumbe walizuru siku ya Ijumaa. 

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, hapa kwenye jukwaa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 22, 2021.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS, hapa kwenye jukwaa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 22, 2021. AFP - JOHN ANGELILLO
Matangazo ya kibiashara

Katikati ya mijadala hiyo, kutakuwa pia na mjadala kuhusu kipindi cha mpito nchini Mali, kwani mvutano umeongezeka katika siku za hivi karibuni kati ya ECOWAS na utawala wa kijeshi.

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea katika siku za hivi karibuni kati ya Accra na miji mikuu ya nchi za jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS. Mamlaka ya Ghana, ambayo ni mwenye kiti wa ECOWAS kwa sasa, imeshauriana na wakuu wa nchi kuandaa kwa haraka mkutano wa kilele kuhusu maendeleo nchini Mali na Guinea.

Marais hao hatimaye wametoa idhni na tarehe sasa imepangwa: mkutano huo utafanyika Novemba 7 mjini Accra, kulingana na vyanzo kadhaa. Siku hiyo,  itajadiliwa suala la kipindi cha mpito nchini Guinea, wakati uhusiano na Conakry unaonekana kutulia kwa kiasi fulani. Wakati huo pia uko Mali itajadiliwa.

Akizuru Bamako tarehe 17 Oktoba, rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alitoa ujumbe kuhusu mamlaka kuheshimu kalenda ya uchaguzi. Uchaguzi wa urais na wa wabunge umepangwa kufanyika Februari 27. Hata hivyo, utawala wa kijeshi wammekuwa wakibaini kwamba wanaandaa majadiliano ya kitaifa kabla ya kupanga tarehe ya uchaguzi. Mvutano huo uliongezeka wiki hii na baada ya Bamako kmfukuza mwakilishi wa ECOWAS siku ya Jumatatu.

Jibu kutoka utawala wa kijeshi unasubiriwa Jumapili hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.