Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Kanali Doumbouya hakubaliani na suala la mpatanishi wa ECOWAS

Mkutano wa mwisho wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kuhusu migogoro ya Guinea na Mali, ambao ulifanyika mwishoni mwa juma lililopita mjini Accra, ulimtaja mjumbe maalum wa Tume hiyo nchini Guinea.

Kanali Mamadi Doumbouya (miwani myeusi), kigogo wa Conakry. Septemba 10, 2021.
Kanali Mamadi Doumbouya (miwani myeusi), kigogo wa Conakry. Septemba 10, 2021. REUTERS - SALIOU SAMB
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ibn Chambas, mwanadiplomasia wa Ghana, ameteuliwa kuwa mpatanishi kati ya jumuiya hiyo ya kikanda na Guinea, iliyowekewa vikwazo na ECOWAS kwa kuchukuwa madaraka kwa nguvu. Lakini mamlaka nchini Guinea inabaini kwamba hakuna mgogoro wa ndani na kwamba mchakato wa mpito uko kwenye njia sahihi. Hii ndiyo sababu Kanali Mamadi Doumbouya, kiongozi mkuu wa mapinduzi huko Conakry, alimwandikia mkuu wa nchi wa Ghana, rais wa sasa wa ECOWAS.

Katika barua hii, rais wa mpito na Mkuu wa Nchi ya Guinea ameandika: "Nimepokea hatua ya viongozi wa kikanda kutambua hatua iliyopigwa katika mchakato wa mpito nchini Guinea. Ameongeza: “Napenda kusisitiza dhamira yangu ya kufanya kila liwezekanalo ili kuendeleza mchakato huu kwa umoja na kwa pamoja, kwa kuzingatia masharti ya katiba ya mpito ambayo ndiyo Katiba ya muda. "

Kanali Doumbouya anasisitiza "utayari wa serikali ya Guinea kudumisha mazungumzo ya mara kwa mara na ushirikiano wa karibu na ECOWAS wakati wa akipindi hiki cha mpito".

Hata hivyo, ameandika, "uteuzi wa mjumbe maalum hauonekani kwetu kuwa wa mwafaka au wa dharura kwani hakuna mgogoro wowote ambao umeonekana ambao unaweza kuhatarisha mwenendo wa kawaida kipindi cha mpito".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.