Pata taarifa kuu
SUDAN-MAKABILIANO

Sudan: Vifo vyaongezeka huko Darfur baada ya makabiliano ya kikabila

Nchini Sudan, idadi ya vifo kufuatia makabiliano kati ya makabila hasimu latika jimbo la Darfur Magharibi mmwa Sudan wikendi hii inaendelea kuongezeka. Takriban watu 48 waliouawa kulingana na chama cha madaktari. Zaidi ya idadi hiyo kulingana na viongozi wa eneo hilo ambao wamebaini kwamba watu 90 waliuawa.

Katika jimbo la Darfur, ghasia hutokea mara kwa mara kati ya makabila ya Waarabu na wasio Waarabu kuhusiana na mzozo wa ardhi na maliasili katika eneo hilo.
Katika jimbo la Darfur, ghasia hutokea mara kwa mara kati ya makabila ya Waarabu na wasio Waarabu kuhusiana na mzozo wa ardhi na maliasili katika eneo hilo. © Abdulmonam Eassa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hili ni tukio la pili la mauaji kutokea katika kipindi cha wiki tatu katika eneo hili. Mapigano hayo yalianza siku ya Jumamosi kufuatia mabishano kati ya makabila mawili hasimu, yapata kilomita 30 mashariki mwa El-Genaïna.

Kama chanzo cha vurugu hizo, mabishano ya Jumamosi jioni kati ya muuzaji wa simu za rununu na mteja wake. Mzozo huo ulipungua haraka na kuwa mapigano kati ya watu wa jamii mbili, kabila la Waarabu upande mmoja na kabila la Waafrika kwa upande mwingine.

Kulingana na mashahidi kadhaa, watu wenye silaha wa wanamgambo wa Kiarabu Janjaweed walishambulia kambi ya ya wakimbizi wa ndani ya Kreinik, na kuchoma moto nyumba kadhaa. Kulingana na gavana wa jimbo hilo, mapigano hayo ya Jumapili yalidumu zaidi ya saa saba kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa kumi jioni. Yalikuwa mapigano makali kiasi kwamba mamlaka ilituma askari wa serikali kwenye eneo la tukio.

Watu 50 wauawa  baada ya mzozo kuhusu wizi wa ngamia

Wiki tatu zilizopita, ghasia kati ya wafugaji wakishtumiana wizi wa ngamia zilisababisha vifo vya watu 50 na moto na nyumba 594 zilichomwa moto, kulingana na Umoja wa Mataifa. Eneo hili linakumbwa mara kwa mara na mapigano yanayosababishwa hasa na mizozo ya ardhi au matatizo ya upatikanaji wa maji, na migogoro kati ya makabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.