Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Hamdok kujiuzulu wakati wowote

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amelifahamisha kundi la wahusika wa kisiasa na wasomi nchini humo kwamba anapanga kujiuzulu saa chache zijazo, shirika la habari la REUTERS limebaini likinukuu watu wawili walio karibu na kiongozi huyo siku ya Jumanne.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, hapa ilikuwa Februari 14 , 2020 huko Berlin, Ujerumani.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, hapa ilikuwa Februari 14 , 2020 huko Berlin, Ujerumani. REUTERS - HANNIBAL HANSCHKE
Matangazo ya kibiashara

Abdallah Hamdok aliyetimuliwa madarakani Oktoba 25 baada ya jeshi kufanya mapinduzi,  alirejea madarakani mwezi uliopita kama sehemu ya makubaliano ya kisiasa na serikali ambayo yalizua wimbi jipya la maandamano.

Maelfu kadhaa ya watu waliingia tena mitaani siku ya Jumamosi katika mji mkuu wa Khartoum kukataa utawala wa jeshi na kurejea kwa Abdalla Hamdok, uamuzi ambao bwana Hamdok alisema aliuchukua ili kulinda mafanikio ya kidemokrasia yaliyopatikana wakati wa kipindi cha mpito na kumaliza "umwagaji wa damu".

Ukandamizaji dhidi ya maandamano yanayopinga utawala wa kijeshi umesababisha vifo vya watu 47, wakiwemo wawili katika maandamano ya Jumamosi.

Duru za karibu na Abdalla Hamdok zilidokeza siku za nyuma kuwa waziri mkuu alinuia kusalia madarakani iwapo tu atakuwa na uungwaji mkono wa kisiasa na kwamba masharti ya makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa kijeshi yataheshimiwa.

Makubaliano hayo yanataka hasa kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa na kuruhusu mkuu wa serikali kuteua mawaziri wake kwa uhuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.