Pata taarifa kuu

Sudan: Makabiliano makali yatokea kati ya majeshi ya Ethiopia na Sudan

Hali ni tete kwenye mpaka kati ya Sudan na Ethiopia. Jeshi la Sudan limeshutumu, Jumamosi, Novemba 28, shambulio lililotekelezwa na vikosi vya Ethiopia katika eneo linalozozaniwa la al-Fashaga, ikiwa ni hatua ya mvutano kati ya nchi hizo mbili kwa miaka mingi. 

Vikosi vya jeshi vikiwa njiani kutoka Khartoum kuelekea katika Jimbo la Gedaref vitumwa kwenye mpaka wa Ethiopia. Malori yakiwa na askari na magari ya kivita.
Vikosi vya jeshi vikiwa njiani kutoka Khartoum kuelekea katika Jimbo la Gedaref vitumwa kwenye mpaka wa Ethiopia. Malori yakiwa na askari na magari ya kivita. Nicolas Cortes - Nicolas Cortes
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Sudan linabainisha kuwa shambulio hili lilisababisha vifo vya watu kadhaa miongoni mwa wanajeshi wake, bila kutaja idadi.

Jeshi la Sudan linaeleza kuwa vikosi vyake vinavyolinda mazao katika eneo hili la al-Fashaga vimeshambuliwa na jeshi la Ethiopia na wanamgambo. Jeshi la Sudan limesema shambulio hilo limelenga kuwatishia wakulima na kuhujumu msimu wa mavuno.

Jeshi la Sudan limethibitisha kwamba shambulio hilo limezuiwa na wanajeshi wake lakini pia linataja hasara kubwa za kibinadamu na mali, bila kutoa maelezo zaidi juu ya matokeo. Mamlaka ya Ethiopia haikutoa maelezo yoyote.

Hii si mara ya kwanza kwa mapigano kutokea katika eneo kubwa la al-Fashaga, lenye ardhi yenye rutuba. Mapigano hutokea mara kwa mara katika eneo hilo. Yaliongezeka mwaka jana wakati mzozo kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na mamlaka huko Tigray ulisababisha makumi ya maelfu ya Waethiopia kutafuta hifadhi mashariki mwa Sudan. NI pia baada ya kuanza kwa mzozo huu, huko Tigray, ambapo wanajeshi wa Sudan walitumwa katika eneo la al-Fashaga.

Sudan na Ethiopia hazijawahi kuafikiana juu ya mkondo wa mpaka wao, licha ya vikao vingi vya mazungumzo. Nchi hizo mbili pia zinapinagana, kwa zaidi ya miaka kumi, juu ya swali la bwawa kubwa la kuzalisha umeme lililojengwa na Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.