Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Jeshi latumia nguvu kusambaratisha mandamano Sudan

Maafisa wa usalama nchini Sudan, wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika Ikulu ya rais jijini Khartoum, kuendelea kushinikiza jeshi kuacha uongozi wa serikali.

Jeshi la Sudan limetumwa katika mji wa Khartoum ili kujaribu kutuliza maandamano baada ya mapinduzi.
Jeshi la Sudan limetumwa katika mji wa Khartoum ili kujaribu kutuliza maandamano baada ya mapinduzi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji tangu, Oktoba tarehe 25, wamekuwa wakiendeleza maandamano ya mara kwa mara, wakati jeshi likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan lilipoamua kuchukua madaraka kutoka kwa Waziri Mkuu wa kiraia Abdalla Hamdok.

Waandamanaji walifurika nje ya Ikulu ya rais, licha ya ulinzi mkali uliokuwa umewekwa na maafisa wa usalama jijini Khartoum, huku jeshi lilikata mawasiliano ya simu na kufunga Internet, saa chache kabla ya kuanza kwa maandamano hayo.

Mpaka sasa, karibu watu 50 wameauwa katika maandamano haya kwa mujibu wa Kamati huru ya Madaktari, huku wengine wakijeruhiwa, wakati huu, uongozi wa jiji la Khartoum, ikionya kuwa itawachukulia hatua kali kwa yeyote atakayeleta fujo.

Kumekuwa na ripoti kuwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ambaye alirejeshwa madarakani na jeshi, baada ya kutia saini mkataba wa kisiasa, huenda akaachia nafasi hiyo kwa kile anachokisema, hapati ushirikiano kutoka kwa raia.

Waandamanaji wanasema, hawataacha kuandamana hadi pale, jeshi litakapoachia madaraka na kuruhusu raia kuongoza nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.