Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Kwa nini Abdallah Hamdok anashindwa kuunda serikali

Baada ya maandamano makubwa ya kupinga mapinduzi ya kijeshi, hali ya kisiasa bado inaonekana si ya uhakika nchini Sudan. Waziri Mkuu Abdallah Hamdok amerejea kwenye wadhifa wake, yapata mwezi mmoja sasa na bado hakuna serikali iliyoundwa kufikia sasa. Kazi yake inaonekana kuwa ngumu zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Serikali ya Sudan, akiwemo Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, ilifikia makubaliano ya amani na waasi.
Serikali ya Sudan, akiwemo Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, ilifikia makubaliano ya amani na waasi. AFP
Matangazo ya kibiashara

yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye watu wake pia walikuwa wamewaweka kizuizini takriban wawakilishi wote wa kiraia wa kipindi cha mpito cha Sudan. Akiwa katika kizuizi cha nyumbani kwa wiki kadhaa, mwanauchumi huyu wa zamani wa Tume ya Afrika ya Umoja wa Mataifa, wakati huo alitetewa sana kupitia maandamano ya kiraia wakidai aachiliwe huru. Lakaini baada ya kuachiliwa kwake, kiongozi huyo wa kiraia alitiwa saini Novemba 21 kwa makubaliano yenye utata na viongozi wa kijeshi, jambo ambali liliwaghadhabisha raia na kumiminika tena mitaani.

"Makosa makubwa ya kisiasa"

Jenerali Burhan alimrejesha Abdallah Hamdok kwenye wadhifa wake kwa kumtaka aunde serikali kwa kusubiri uchaguzi ulioahidiwa na jeshi mmwezi Julai 2023. Makubaliano haya yalionekana kama usaliti na sehemu kubwa ya kambi inayounga mkono demokrasia na vyama vingi vya kisiasa na asasi za kiraia. Kwa mujibu wa mkataba aliotia saini na viongozi wa kijeshi, Abdallah Hamdok lazima kwanza afanye mashauriano ya kisiasa na wawakilishi mbalimbali wa vyama kabla ya kuunda serikali.

Lakini Waziri Mkuu ametengwa. Ni timu ndogo tu ya wasomi au mawaziri wa zamani wamebaki waaminifu kwake. "Alifanya makosa makubwa ya kisiasa," anasema Yassir Arman, mshauri wake wa zamani ambaye amejitenga naye. Amebaini kwamba Abdallah Hamdok hana uwezo wa kutengua maamuzi yaliyochukuliwa na Jenerali Burhan, yakiwemo mamia ya uteuzi wa walio karibu na jeshi kushika nyadhifa muhimu katika utawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.