Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Maelfu wamiminika mitaani kupinga utawala wa kijeshi Sudan

Maelfu ya waandamanaji walijotokeza jana jijini Khartoum, kuendelea kutaka serikali ya kiraia, baada ya jeshi kuchukua madaraka nchini humo.

Wasudan waandamana kuelekea ikulu ya rais huko Khartoum, Desemba 19, 2021.
Wasudan waandamana kuelekea ikulu ya rais huko Khartoum, Desemba 19, 2021. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama walitumia mabamu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji ambao kwa mwaka wa tatu baada ya kumwondoa kiongozi wa zamani Omar Al Bashir, wameendeleza maandamano.

Maafisa wa usalama walitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji, waliokuwa wamefika mbele ya Ikulu ya rais.

“Huu ni uthibitisho kuwa watu wa Sudan ni imara.Tunaweza kuuangusha uongozi huu kama tulivyofanya kwa ule uliopita. Ni uthibitisho kuwa mateso hayaturudushwi nyuma. Lazima maamuzi ya wananchi yaheshimiwe, hatutakubali kuongozwa na mtu amabye haheshimu uamuzi wa watu, “ amesema mmoja wa waandamanaji.

“Wanawaua watoto wetu na kutupiga. Burhane, Hemetti, Kabashi ni magaidi na Hamdok ameugana nao.Tunataka kuongozwa na raia. Tunataka asilimia 100 ya uongozi wa kiraia. Hakuna mjadala katika hilo na hakuna ushirikiano katika hili. Sikiliza tunashinikiza hili, “ amesema mandamanaji mwengine.

 Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini kwa kutumia pikipiki, huku waandamanaji wakisema hawahofu lolote na wataendelea na maandamano kushinikiza kupatikana kwa serikali ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.