Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Wachambuzi : Kurejeshwa kwa Hamdok kwenye wadhifa wake ni kama kuwafumba macho raia

Wachambuzi wa masuala ya Sudan wanaonya kuwa, licha ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok kurejeshewa madaraka, bado yupo chini ya huruma ya wanajeshi na kilichotokea ni kama kusafisha mapinduzi yaliyotokea.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, aliyetimuliwa kwenye wadhifa wake wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25, amerejeshwa kwenye wadhifa huo Jumapili, Novemba 21, 2021 baada ya makubaliano na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, yaliyotiwa saini katika Ikulu ya rais mjini Khartoum, mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, aliyetimuliwa kwenye wadhifa wake wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25, amerejeshwa kwenye wadhifa huo Jumapili, Novemba 21, 2021 baada ya makubaliano na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, yaliyotiwa saini katika Ikulu ya rais mjini Khartoum, mbele ya waandishi wa habari. © Photo fournie par le Conseil souverain de transition soudanais, via AP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Hamdok kurejeshewa madaraka kwa kiasi kikubwa inaaminiwa ni kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya kimataifa kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa za Sudan.

Magdi al-Gizouli, mtalaam wa Sudan kutoka taasisi ya Rift Valley anasema, jeshi halikufuta hatua ya kuchukua madaraka licha ya kutangaza kumrejesha Hamdok kwenye wadhifa wake.

Tangu jeshi lilipotangaza kuchukua madaraka mwezi mmoja uliopita, Hamdok alikuwa kwenye kifungo cha nyumbani.

Al-Gizouli anaona kuwa hata Baraza la Mawaziri litakaloteuliwa na Hamdok, litakuwa mikononi mwa wanajeshi na huenda likapata shinikizo mara kwa mara.

Hata hivyo, hatua ya Hamdok kurejeshewa madaraka imepongezwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na pamoja na Saudi Arabia na Misri, nchi ambazo zina uhusiano wa karibu na jeshi nchini Sudan.

Marekani na Uingereza pia zimepongeza Abdalla Hamdok kurejeshewa madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.