Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Sudan yaendelea kukumbwa na maandamano ya kiraia

Sudan imeendelea kukabiliwa na maandamano ya kiraia tangu jeshi lilipo twaa madaraka baada ya kumpindua waziri mkuu Abdalla Hamdok na serikali yake pamoja na kusitisha shughuli za Bunge.

Raia wanaounga mkono demokrasia wanaendelea na maandaano nchini Sudan wakitaka utawala wa kiraia.
Raia wanaounga mkono demokrasia wanaendelea na maandaano nchini Sudan wakitaka utawala wa kiraia. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama na jeshi vimeendelea kukabiliana na umati wa waandamanaji, huku baadhi ya waandamanaji wakiuawa, kujeruhiwa na wenginekukamatwa.

Siku ya Jumatatu wiki hii maafisa wa usalama mwalitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha mamia ya waandamanaji waliofurika katika Ikulu ya rais jijini Khartoum, kushinikiza uongozi wa kiraia.

Maandamano kama haya yamekuwa yakiendelea katika wiki kadhaa sasa, kupinga serikali ambayo kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na jeshi.

Baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi Oktoba, baadaye iliamua kuingia kwenye mkataba na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok mwezi Novemba, baada ya shinikizo kutoka ndani na nje, hatua ambayo iliwakera raia wa nchi hiyo.

Mbali na Khartoum, maandamano pia yameshuhudiwa katika majimbo ya Mashariki mwa nchi hiyo ya Kassala na Gedaref, wakipeperusha bendera za nchi hiyo.

Uongozi wa kijeshi nchini humo, umeendelea kujitetea kuwa hatua ya kuchukua madaraka mwezi Oktoba, haukuwa mapinduzi bali mchakato wa kuingoza Sudan kufikia mfumo wa demokrasia, huku ikiahidi kuwa uchaguzi utafanyika mwezi Julai mwaka 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.