Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: ECOWAS yataka uchaguzi kufanyika mwezi Februari na yatishia vikwazo vipya

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwa kauli moja wameamua uchaguzi kufanyika Februari 27 nchini Mali. Viongozi hao wakikutana Jumapili hii, Desemba 12 katika mkutano wa kawaida wa kilele huko Abuja, nchini Nigeria, kuhusu hali ya Mali

Wakati wa zoezi la uhesabuji kura kuhusiana na uchaguzi wa urais nchini Mali,  Agosti 18, 2018 mjini Bamako.
Wakati wa zoezi la uhesabuji kura kuhusiana na uchaguzi wa urais nchini Mali, Agosti 18, 2018 mjini Bamako. AP - Annie Risemberg
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya hiyo ya kikanda inatishia kupigia kura vikwazo vipya mwezi Januari 2022 ikiwa hali haitabadilika. Hitimisho hili lilisubiriwa kwa hamu huko Bamako na kusababisha vyama vya kisiasa kujibu.

Jumapili, Desemba 12, ECOWAS, ambayo ilichukuwa uamuzi wa kuisimamisha Mali katika taasisi zake, inaendelea kudumisha shinikizo kwa nchi hiyo, bila hata hivyo kutangaza vikwazo vipya. Wakuu wa nchi tisa walioshiriki mkutano huo, walionyesha umoja na msimamo wao, amepoti Serge Daniel, mwanahabari wetu maalum huko Abuja. "Tulibaini kwamba ifikapo mwisho wa mwezi Desemba 2021 hivi karibuni, tuweze kuwa na hatua sahihi zaidi na madhubuti ambazo zitachukuliwa na ambazo zinaonyesha kuwa tuko katika harakati za kuona uchaguzi unafanyika mwezi Februari 2022", alisema Jean-Claude Kassi Brou, mwenyekiti wa ECOWAS.

Bamako itakabiliwa na vikwazo vipya "mwanzoni mwa mwezi wa Februari" ikiwa hali haitobadilika, aliongeza mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS. Hili ni onyo lakini sio vikwazo; uamuzi ambao ni ishara wa vitisho amesema Jeanmille Bittar, msemaji wa vuguvugu la Juni 5-Rally of Patriotic Forces (M5-RFP) na ambaye ni mshirika wa karibu wa mamlaka ya sasa.

"Mamlaka na ECOWAS wanajua kuwa kuanzia mwezi Januari, watakuwa na ratiba, amebaini Kaourou Magassa, mwandishi wetu wa habari huko Bamako. Na ikiwa wataamua kushikilia msimamo wao mwezi Januari, inaweza kubadili mambo. Ni kama huko Guinea, tuko katika mchakato wa ujenzi upya. Ikiwa ECOWAS hii inataka kuisaidia Mali, lazima waongeze juhudi za kurejesha usalama. "

Ujumbe wa ECOWAS utazuru Bamako hivi karibuni ili kuwasilisha rasmi ujumbe uliotangazwa Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.