Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Waziri Mkuu wa Mali na mawaziri wake wote walengwa na vikwazo vya ECOWAS

Waziri Mkuu wa Mali Choguel Kokalla Maïga na takriban serikali yake yote ni miongoni mwa watu 149 waliolengwa na vikwazo vya kibinafsi vilivyowekwa hivi karibuni na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Waziri Mkuu wa Mpito wa Mali Choguel Maïga mjini New York, Septemba 26, 2021.
Waziri Mkuu wa Mpito wa Mali Choguel Maïga mjini New York, Septemba 26, 2021. © AFP - KENA BETANCUR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mpito Kanali Assimi Goïta ayumo kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Tume ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), kulingana na waraka rasmi kutoka jumuiya hiyo ya kanda ya magharibi, ambayo shirika la habari la AFP na RFI walipata Jumatano Novemba 17.

Kwa upande mwingine, ndani ya serikali ya Mali, takriban wajumbe wote wa serikali isipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop wana wasiwasi. Waziri Mkuu Choguel Maïga ambaye anaoongoza kwenye orodha hiyo na wote walio na nyadhifa kuu pia wamewekewa marufuku ya kusafiri na kuzuiwa kwa mali za kifedha.

Vikwazo hivyo vinatumika kwa wajumbe wa Baraza la Kitaifa la Mpito (CNT, chombo cha kutunga sheria). Majina ya rais wa CNT na washirika wake wakuu pia yako kwenye orodha ya watu wanaotuhumiwa "kuzuia kurudi kwa utaratibu wa kitaasisi".

Orodha yatolewa wito kurekebishwa

Vyanzo vilivyo karibu na ECOWAS, vinabaini kwamba ili kutumia hatua hizi, msaada wa taasisi za kimataifa utaombwa. Kwa jumla, watu 149 wa Mali wanakabiliwa na vikwazo hivi vilivyochukuliwa.

Kulingana na taasisi ya kikanda iliyohojiwa na RFI, orodha hiyo inaweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya hali nchini Mali. Kwa maneno mengine, inaweza kurefushwa au watu waliolengwa wanaweza kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatimaye, kulingana na afisa wa ECOWAS aliyehojiwa na RFI, orodha ya ndugu ya wale waliochukuliwa vikwazo inaandaliwa.

Vikwazo vya mtu binafsi Novemba 7

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, waliokutana katika mkutano wa kilele tarehe 7 Novemba, waliamua kuwawekea vikwazo watu binafsi ambao, baada ya mapinduzi mawili ya serikali katika mwaka mmoja katika nchi iliyotumbukia katika mgogoro mkubwa, ambavyo vinaweza kuchelewesha uchaguzi ili raia kurejea madarakani. Hata hivyo, kuheshimishwa kwa ratiba hii ilikuwa ni sharti la ECOWAS, ambayo ilikuwa imeondoa vikwazo vyake vya kifedha na biashara dhidi ya Mali, tangu mapinduzi ya kwanza mnamo Agosti 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.