Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: Umoja wa Ulaya waungana na ECOWAS

Umoja wa Ulaya unataka kuchukuwa msimamo dhidi ya utawala wa kijeshi kutokana na mapinduzi ya kijeshi nchini Mali. Unajiandaa kutoa vikwazo baada ya vile vilivyotolewa na ECOWAS Novemba 7.

Bendera za Umoja wa Ulaya mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya huko Brussels.
Bendera za Umoja wa Ulaya mbele ya makao makuu ya Tume ya Ulaya huko Brussels. AFP - JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Diplomasia ya Umoja wa Ulaya imetoa pendekezo la Ufaransa kwa nchi 27 wanachama wa umoja huo. Vikwazo hivyo viko tayari, ni lazima vikamilishwe.

Hakuna tena kusubiri kwa sasa kuchapishwa kwa vikwazo katika siku chache zijazo kwenye Jarida rasmi la Umoja wa Ulaya ili kujua kwa hakika ni nani atakayelengwa nchini Mali. Kama ilivyo kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), wazo ni kuwawekea vikwazo wale wote waliohusika na kucheleweshwa kwa kuandaa uchaguzi.

Marufuku ya kusafiri katika eneo la Schengen na kuzuiwa kwa mali

Umoja wa Ulaya unakataa kusema rasmi ni nani aliye kwenye orodha ya vikwazo, lakini lengo la umoja huo ni kuunga mkono kikamilifu Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). Kwa hivyo wanapaswa kufuata mfano wa ECOWAS na wanaweza kulenga mamlaka zote za mpito nchini Mali.

Kinadharia, hivi vitakuwa vikwazo vya zamani vya Umoja wa Ulaya, ambavyo ni marufuku ya visa kwa ukanda wa Schengen na kuzuiwa kwa mali hususan fedha zilizowekwa katika moja wapo ya nchi mwanachamawa Umoja wa Ulaya.

Shughuli nchini Mali na katika eneo la kampuni ya mamluki ya Urusi Wagner pia itaathiriwa na vikwazo vya Ulaya hivi karibuni. "Kampuni hii inatekeleza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa niaba ya wengine. Na zaidi ya hayo, hutumia moja kwa moja katika nchi na kuendeleza vitendo vya unyanyasaji pamoja na ukiukwaji wa mara kwa mara [wa haki za binadamu]. Kuna tishio la kuingilia kati nchini Mali, amebaini Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa. Na Umoja wa Ulaya umeamua kuichukua vikwazo dhidi ya kampuni ya Wagner: wanachama wa kampuni na makampuni ambayo yanafanya kazi moja kwa moja na kampuni hii ya Wagner. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.