Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: Orodha ya waasi wanaohusika na msamaha wa rais yajulikana

Serikali ilitangaza mapema wiki hii kwamba sheria ya msamaha itapitishwa ili kuruhusu wanachama wa makundi ya kisiasa na kijeshi kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Orodha ya kwanza iliyovuja kwenye mitandao ina majina 254 akiwemo Timan (pichani) na Tom Erdimi, wapwa wa rais wa zamani wa Chad Idriss Deby Itno ambao wamechukua silaha dhidi yake kwa zaidi ya miaka 15.
Orodha ya kwanza iliyovuja kwenye mitandao ina majina 254 akiwemo Timan (pichani) na Tom Erdimi, wapwa wa rais wa zamani wa Chad Idriss Deby Itno ambao wamechukua silaha dhidi yake kwa zaidi ya miaka 15. (Photo : Laurent Correau/ RFI)
Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya sheria mbili zinapaswa kuwasilishwa kwa Baraza la Kitaifa la Mpito, bunge la muda, kwa madhumuni haya. Kwa kusubiri kurasimishwa kwake, orodha ya kwanza imevuja.

Ni waraka wa kurasa tisa unaoitwa "Mswada unaotoa msamaha wa jumla kwa vitendo vya ugaidi, kula njama, kuajiri na kusajili watoto wadogo katika makundi yenye silaha" ambao ulivuja kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi jioni.

Waraka huo una majina 254 yakiwemo Timan na Tom Erdimi, wapwa wa Rais wa zamani Idriss Deby Itno ambao wamechukua silaha dhidi yake kwa zaidi ya miaka 15.

Orodha nyingine inatarajiwa na itahusu karibu watu 300, idadi ya wanachama wa makundi ya upinzani ya kisiasa na kijeshi waliohukumiwa na mahakama ya Chad baada ya mashambulizi dhidi ya utawala wa hayati Marshal Idriss Deby Itno.

Lakini orodha hizo mbili zinatatua sehemu tu ya suala la kisiasa na kijeshi, mchambuzi mmoja amebaini. Wapo walioshika silaha lakini hawakuhukumiwa. Kwa upande wa watu hao, italazimika kutolewa msamaha maalum, kimeongeza chanzo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.