Pata taarifa kuu
CHAD-MAZUNGUMZO

Kiongozi wa waasi wa Chad Erdimi: ‘Nitarejea Ndjamena kutakapokuwa na mazungumzo’

Chad ndiyo kwanza imeanza hatua ya kwanza ya mchakato wa amani iliyoahidiwa na serikali ya mpito. Katika muda wa siku kumi zilizopita, kamati maalum ya kiufundi inayoongozwa na rais wa zamani Goukouni Oueddei imekutana na upinzani pamoja na waasi ili kuanzisha mazungumzo jumuishi ya kitaifa.

Kiongozi wa UFR, Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur.
Kiongozi wa UFR, Timan Erdimi mwaka 2009 huko Darfur. © GUILLAUME LAVALEE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mikutano hiyo ilifanyika katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Paris, Cairo, na Doha. Jumla ya makundi 18 ya kisiasa na yale yaliyochukua silaha yalishiriki katika mikutano hiyo.

Timan Erdimi, ambaye anaongoza chama cha Rally of Forces for Change (RFC) pamoja na UFR, muungano wa makundi kadhaa ya waasi, alihukumiwa kifo nchini mwake na anaishi Qatar kwa zaidi ya miaka kumi. Siku ya Jumatatu, Novemba 1, alikutana na wajumbe wa kamati ya kiufundi huko Doha.

Timan Erdimi amesema yuko tayari kurejea nchini ikiwa atahakikishiwa usalama wake. "Nitarejea Ndjamena kutakapokuwa na mazungumzo."

Awali Timan Erdimi, ameweka masharti yake kwa kushiriki katika mashauriano hayo.

Kiongozi wa UFR alieleza kwamba haoni umuhimu wowote kwenye mazungumzo ya Ndjamena "ambapo hakuna jipya litakalotokea".

Badala yake, UFR inataka mashauriano kati ya makundi ya kisiasa na kijeshi na mamlaka, na kuweka masharti ikiwa ni pamoja na msamaha wa jumla, kurejeshwa kwa mali iliyotwaliwa na kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa, hali sawa na zile za makundi mengine ya kisiasa na kijeshi yaliyokutana huko Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.