Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: serikali yatangaza msamaha wa jumla kwa waasi waliofungwa au walio uhamishoni

Kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri, msamaha wa jumla kwa waasi waliofungwa au walio uhamishoni umetangazwa Jumatatu hii Novemba 29.

Jenerali Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la mpito la kijeshi nchini Chad, alipozuru Khartoum, Sudan, Agosti 29, 2021.
Jenerali Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la mpito la kijeshi nchini Chad, alipozuru Khartoum, Sudan, Agosti 29, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa moja kwa moja katika taarifa ya habari ya televisheni ya serikali na msemaji wa serikali. Msamaha huo unahusu wale wote waliopatikana na hatia ya kukiuka uadilifu wa serikali na pia ukweli unaohusiana na uhuru wa maoni. Msamaha huu unahusu watu 39.

Waziri huyo pia ametangaza msamaha wa jumla kwa wale waliopatikana na hatia ya vitendo vya ugaidi, kushiriki katika ugaidi na kusajili watoto wadogo katika makundi yenye silaha. Wakati huu, uamuzi huu unahusu, kulingana na mamlaka, zaidi ya raia 250 wa Chad waliohukumiwa na Mahakama ya Jinai ya NDjamena ambao walisikilizwa katika gereza la Koro Toro Agosti 22, 2019.

Hii ni ishara ya uwazi kwa upande wa mamlaka kwani msamaha huo ulikuwa moja ya matakwa ya viongozi wa makundi ya kisiasa yenye silaha kwa ushiriki wao katika mazungumzo ya kitaifa, ambayo tarehe yake bado haijatajwa.

Ombi hili lilitolewa wakati wa mashauriano kati ya viongozi wa makundi ya waasi na wajumbe wa kamati maalum ya kiufundi inayoongozwa na rais wa zamani Goukouni. Mashauriano haya yalifanyika nchini Qatar, Ufaransa na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.