Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: Mahamat Idriss Déby adai yuko njia nzuri kutimiza ratiba ya mpito

Rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi nchini Chad Mahamat Idriss Déby anaamini kuwa yuko katika "wakati mzuri" kutimiza ratiba ya mpito na ameahidi kuwa uchaguzi utakuwa "huru wa kidemokrasia na wa kuaminika". Mahamat Idriss Déby alizungumza jana Ijumaa usiku kwenye televisheni ya France 24, wakati wa ziara yake huko Paris.

Wakati wa mahojiano, Mahamat Idriss Déby (picha yetu ya kielelezo) alianza kwa kutejitea kuingia kwake madarakani: “Mapinduzi yanapangwa mapema. Na kile kilichotokea Chad, hakuna mtu angelieza kutarajia kuwa kingelitokea.
Wakati wa mahojiano, Mahamat Idriss Déby (picha yetu ya kielelezo) alianza kwa kutejitea kuingia kwake madarakani: “Mapinduzi yanapangwa mapema. Na kile kilichotokea Chad, hakuna mtu angelieza kutarajia kuwa kingelitokea. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Takriban miezi saba baada ya kuingia madarakani, kufuatia kifo cha babake, alizungumzia changamoto zinazoikabili nchi yake.

"Mapinduzi yanapangwa mapema. Na kile kilichotokea Chad, hakuna mtu angelieza kutarajia kuwa kingelitokea. Mahamat Idriss Déby alianza kwa kutetea juingia kwake madarakani: yeye si hakufanya mapinduzi, alichukua majukumu chini ya hali ya kipekee. "Hakuitwa" na Ufaransa, lakini Paris "ilielewa chaguo hili", aliongeza.

Chad inakabiliwa na vitisho kadhaa. Kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi katika uknda wa Sahel, amesema jeshi lake halitaondok: “Chad imejitolea kupambana na ugaidi. Na hadi leo, tunapigana vita hivi. Majeshi ya Afrika yanaweza kukabiliana na ugaidi. "

"Kutekeleza" ahadi

Ndani ya nchi, rais wa Baraza la Mpito la Kijeshi (CMT) alitetea mchakato unaoendelea wa mpito, na anaamini yuko "katika wakati unaofaa" kutimiza ratiba ya miezi 18: "Kwa kuzingatia ramani yetu kuhusiana na uchaguzi , tuko kwenye wakati unaofaa. Kuna utashi wa kisiasa na naamini inawezekana kutimiza ahadi hizo. "

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuwania katika uchaguzi utakaofuata kipindi cha mpito, alikwepa swali: “Wajibu wangu ni mzito sana, hauniruhusu kujifikiria,” amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.