Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: Haroun Kabadi ateuliwa kuwa mkuu wa Baraza la Mpito

Hatimaye Baraza la Taifa la Mpito limetangazwa nchini Chad tangu Jumanne, Oktoba 5. Haroun Kabadi, Spika wa Bunge lililovunjwa siku chache zilizopita, ameteuliwa kuwa mkuu wa baraza hilo, uteuzi ambao haukuwashangaza wengi nchini humo.

Rais wa Baraza la Taifa la Mpito, Haroun Kabadi, Oktoba 5, 2021 huko Ndjamena.
Rais wa Baraza la Taifa la Mpito, Haroun Kabadi, Oktoba 5, 2021 huko Ndjamena. © DJIMET WICHE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Haroun Kabadi, 73, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Mpito, bunge la mpito lililoidhinishwa na serikali ya kijeshi tangu kifo cha Idriss Debly mwezi Aprili. Wagombea wawili, Haroun Kabadi na Delwa Kassiré Coumakoye, ambao wote ni wazowefu na maarufu katika siasa ya Chad, walikuwa wanawawania kwenye nafasi hiyo.

Lakini baada mashauriano, mwenyekiti wa kikao alitangaza kuwa mgombea Kassiré amejiondoa kwenye kinyang'anyiro na kumuachia spika wa zamani wa Bunge kuwania kwenye nafasi hiyo. Dakika chache badaye wabunge walishangilia kwa kupiga makofi, na hivyo kumteua kwa maelewao rais mpya wa bunge la muda.

Kwa upande wake Haroun Kabadi amesema atahakikisha taasisi yake inaifikisha Chad katika uchaguzi wa wazi na usiobagua.

"Lengo letu sio kukinzana na serikali, lakini kuweka mazingira mazuri na kuhakikisha nchi hii inaondokanana kipindi cha mpito na kufanya uchaguzi wa wazi, usiobagua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.