Pata taarifa kuu
ECOWAS-USHIRIKIANO

ECOWAS yaongeza vikwazo dhidi ya wanajeshi walioko madarakani nchini Mali na Guinea

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wameamua kuongeza vikwazo dhidi ya wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali na Guinea. Viongozi walikutana jana Jumapili mjini Accra, nchini Ghana.

Wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Accra, Novemba 7, 2021.
Wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Accra, Novemba 7, 2021. © RFI/Serge Daniel
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa kikao cha faragha, kulingana na habari kutoka kwa mwandishi wetu Serge Daniel, imeelezwa kwenye barua rasmi ambayo serikali ya Mali ilitangaza kwamba haiwezi kufanya uchaguzi wa rais na wabunge mwezi Februari 2022, kama ilivyopangwa hapo awali.

Kuhusu Guinea, Jean-Claude Kassi Brou, rais wa Tume ya ECOWAS, alifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Accra, ambapo alisema kuwa wakuu wa nchi walisisitiza juu ya uharaka wa kumwachilia huru rais wa zamani Alpha Condé, ambaye ni mfungwa wa viongozi wa mapinduzi huko Conakry.

Jambo lingine kuhusu Guinea ni hali ya kipindi cha mpito. Wakuu wa Nchi za ECOWAS wamepokea taarifa ya kurasimishwa kwa Mkataba wa Mpito. Kwa hiyo, hatua nzuri kwa mamlaka ya Guinea. Waziri mkuu wa kiraia ameteuliwa, serikali ya kiraia pia imewekwa na inafahamika kwamba Baraza la Mpito la Kitaifa litawekwa rasmi hivi karibuni.

Lakini wakuu wa nchi za ECOWAS walitaka kuwa na taarifa kamili kuhusiana na hatua ambazo zitapelekea kufanyika kwa uchaguzi. ECOWAS inapendekeza miezi sita kwa ajili ya kuandaa uchaguzi nchini Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.