Pata taarifa kuu
ECOWAS-USHIRIKIANO

ECOWAS kuijadili Mali na Guinea

Mkutano wa kilele wa usiokuwa wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) unafunguliwa Jumapili, Novemba 7 huko Accra, Ghana. Viongozi hao watajadili hali nchini Guinea na Mali, ambapo jeshi lilichukua mamlaka kupitia mapinduzi. Miongoni mwa masuala, vikwazo vya kiuchumi huenda vikachukuliwa dhidi ya nchi hizi mbili.

ECOWAS inaweza kuamua kuchukuwa vikwazo dhidi ya Mali na Guinea katika mkutano wake wa kilele wa tarehe 7 Novemba 2021. Hapa, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, mpatanishi wa Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Septemba 16, 2021.
ECOWAS inaweza kuamua kuchukuwa vikwazo dhidi ya Mali na Guinea katika mkutano wake wa kilele wa tarehe 7 Novemba 2021. Hapa, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, mpatanishi wa Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS mjini Accra, Septemba 16, 2021. AFP - NIPAH DENNIS
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi za ECOWAS wote wana wasiwasi kuhusu hali inayoendelea nchini Mali na Guinea: kurejea kwa utaratibu wa kikatiba nchini Guinea na Mali ni muhimu, pamoja na kuandaa uchaguzi wa uwazi.

Katika miezi michache, kumekuwa na mapinduzi mawili ya kijeshi nchini Mali, moja nchini Guinea. Maafisa wawaili wa vyeo vya Luteni Kanali ndio wanaongoza nchi hizo mbili.

Mjini Accra, majadiliano yatahusu sana muda wa tawala za kijeshi katika nchi hizo mbili. Huko Conakry, tofauti na Bamako, hakuna mapambano ya kweli dhidi ya jeshi na waandamanaji na serikali ya kiraia imeanzishwa, amekumbusha mwandishi wetu wa Conakry. Mabalozi wa nchi wanachama wa ECOWAS mjini Conakry wanatoa wito wa kuelewana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.