Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: ECOWAS yaonyesha msimamo wake mkali dhidi ya rais wa mpito Assimi Goïta

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, rais wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), alifanya ziara nchini Mali Jumapili, Oktoba 17 ili kujionea mwenyewe hali halisi ya maendeleo ya mchakato ambao unapaswa kuindoa nchi hiyo katika mgogoro inayopitia. Alikutana na rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta.

Kanali Assimi Goïta, rais wa mpito wa Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 2020.
Kanali Assimi Goïta, rais wa mpito wa Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 2020. REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo na rais wa Mpito wa Mali Kanali Assimi Goïta walikuwa na vikao viwili vya mazungumzo Jumapili Oktoba 17. Kutlingana na chanzo kiliyoshiriki mikutano hiyo, Kanali Assimi Goïta alielezea hali halisi inayoripotiwa nchini, hususan matatizo yanayoikabili nchi yake, hasa ukosefu wa usalama na mikutano ya kitaifa iliyotangazwa. "Assimi Goïta alizungumza kwa utulivu, kama kawaida yake, lakini kwa uwazi," anasema mmoja wa washirika wake wa karibu.

Katika hatua nyingine kuhusiana na suala lamamluki wa kulipwa kutoka kampuni ya Urusi ya Wagner, alikumbusha kwamba anatafutiwa kisingizio, na kwamba nchi yake bado haijasaini chochote na kampuni hii ya kibinafsi ya Urusi inayotumia mamluki.

Kuheshimisha ahadi kuhusu kufanyika kwa uchaguzi

Kwa upande wake, kulingana na habari zetu, rais wa sasa wa ECOWAS alisema  akikumbusha kwamba wanajeshi wa Mali lazima waheshimu ahadi zao kwa kuandaa uchaguzi wa urais na wa wabunge mwishoni mwa mwezi Februari 2022. Nana Akufo-Addo alikumbusha kwamba kabla ya mwisho wa mwezi wa Oktoba, mamlaka nchini Mali ilikuwa imeahidi kuweka hadharani ratiba ya vitendo vyote vitakavyofanyika hadi mwisho wa kipindi cha mpito hasa kutangaza tarehe ya mwisho ya kipindi cha mpito.

Kulingana na habari zetu, wajumbe wawili kutoka ECOWAS wanatarajiwa kurudi nchini Mali kabla ya mwisho wa mwezi huu ili kuangalia iwapo ahadi hizo zitakuwa zimetekelezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.