Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Ujumbe wa wakuu wa nchi za ECOWAS wawasili Conakry

Jumuiya ya Kuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS inaendelea kuonyesha msimamo wake kwa kupinga kabisa kile kilichotokea nchini Guinea, siku moja baada ya mkutano wa dharurahuko Accra, nchini Ghana.

Ndege ya ujumbe wa Cote d'Ivoire ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Conakry, Guinea, Septemba 17, 2021.
Ndege ya ujumbe wa Cote d'Ivoire ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Conakry, Guinea, Septemba 17, 2021. © RFI/Charlotte Idrac
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa marais wa nchi wanachama wa ECOWAS umewasili jijini Cobakry Ijumaa wiki hii kujadili na viongozi wa mapinduzi.

Siku ya Alhamisi, Septemba 16, 2021, ECOWAS iliamua kuweka vikwazo dhidi ya viongozi wa mapinduzi waliomtimuwa madarakani Alpha Condé Septemba 5, na wanawapa miezi sita kuandaa uchaguzi wa urais na wa wabunge.

Rais wa Ghana ambaye ni rais wa sasa wa ECOWAS, Nana Akufo-Addo, aliwasili leo mchana na mwenzake wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara, katika mji mkuu wa Guinea. Wawili hawa wamepokelewa na Kanali Doumbouya, mkuu wa Kamati ya Kitaifa kwa ajili ya Maendeleo ya Guinea (CNRD). Pia walikuwepo viongozi wa jeshi, mabalozi na gavana mpya wa Conakry.

Lengo la ziara hii ni kuwaarifu maafisa wa CNRD kuhusu maamuzi yaliyochukuliwa Alhamisi katika mkutano wa ECOWAS huko Accra, nchini Ghana, wiki moja tu baada ya ujumbe wa kwanza wa kidiplomasia huko Conakry ambao uliweza kukutana na rais aliyepinduliwa Alpha Condé.

ECOWAS imepaza sauti kudai kurudi kwa utaratibu wa kikatiba nchini Guinea na mabadiliko ya haraka: miezi sita ya kufanya uchaguzi wa urais na wa wabunge. Vikwazo pia vilitangazwa dhidi ya viongozi wa mapinduzi: marufuku ya kusafiri, kufungiawa mali zao na kisha kupiga marufuku wanachama wa CNRD kugombea urais. ECOWAS ni wazi inataka kwenda haraka. Katika taarifa yake, jumuiya hiyo ilionyesha wasiwasi wake juu ya kuibuka tena kwa mapinduzi baada ya yale ya Mali mnamo 2021 na 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.