Pata taarifa kuu
GUINEA

ECOWAS kuijadili Guinea baada ya kumtimua mamlakani Alpha Condé

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inakutana leo Alhamisi hii, Septemba 16, katika mkutano wa dharura ili kuchukuwa uamuzi kuhusiana na kesi ya Guinea, siku kumi na moja baada ya mapinduzi.

Wajumbe wa ECOWAS wakizuru Conakry, Septemba 10.
Wajumbe wa ECOWAS wakizuru Conakry, Septemba 10. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, ECOWAS ilisimamisha Guinea katika taasisi zake zote. Wengi wanajiuliza iwapo ECOWASi itachukuwa hatua zaidi dhidi ya Guinea leo Alhamisi? Mada hii inatarajiwa kutatuliwa. Ili kuwasaidia kuamua, wakuu wa nchi za Afrika Magharibi watakuwa na ripoti ya ujumbe wa ECOWAS uliozuru Guinea Ijumaa ya wiki iliyopita.

Katika ripoti yao, wajumbe wa ECOWAS walitoa mapendekezo kadhaa. Kwanza raia warudishiwe madaraka halafu kipindi cha mpito kiwe kifupi.

Mapendekezo mengine ni pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa na hasa rais aliyeondolewa mamlakani Alpha Condé. Mapendekezo haya yatakuwa kwenye ajenda ya mkutano wa viongozi wa ECOWAS leo Alhamisi.

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, wawakilishi wa ECOWAS pia watajadili hali ya Mali. Marais wa Liberia na Guinea Bissau walikuwa tayari wamewasili Jumatano hii jioni huko Accra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.