Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Mawaziri wanne kuachiliwa huru Sudan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alikutana Alhamisi, Novemba 4 na mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, anayeongoza nchi hiyo tangu mapinduzi ya Oktoba 25 na ambaye anaendelea kumshikilia Waziri Mkuu Abdallah Hamdok.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan katika mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum.
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan katika mkutano na waandishi wa habari Oktoba 26, 2021 mjini Khartoum. © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Antony Blinken amemtaka "kurejesha serikali inayoongozwa na raia," kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

"Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alimtaka Jenerali Burhan kuwaachilia mara moja wahusika wote wa kisiasa waliozuiliwa tangu Oktoba 25 na kurejea kwenye mazungumzo ya kumrejesha Waziri Mkuu Hamdok kwenye wadhifa wake," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ned Price, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alizungumza kwa njia ya simu siku ya Alhamisi (Novemba 4) na mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, akimtaka kurejesha serikali ya mpito ya kiraia, zaidi ya 'wiki moja baada ya mapinduzi. Alitoa wito wa kuachiliwa kwa viongozi wa kiraia waliokamatwa, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, ambaye yuko chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi hayo. Muda mfupi baada ya taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa, jenerali huyo aliamuru kuachiliwa kwa mawaziri wanne wa Sudan, kulingana na televisheni ya taifa.

Kulingana na tangazo lililotangazwa jioni ya Alhamisi, Novemba 4 na televisheni ya serikali, Hamza Baloul, Waziri wa Habari na Utamaduni, Hachem Hassab al-Rassoul, Waziri wa Mawasiliano, Ali Jeddo, Waziri wa Biashara, na Youssef Adam, Waziri wa Vijana na Michezo, wataachiliwa huru. Hakuna tarehe ya kuachiliwa kwao iliyotangazwa. Usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, saa kadhaa baada ya tangazo hilo, hakukuwa na dalili ya kuachiliwa kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.