Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Jeshi latangaza kuundwa kwa serikali mpya hivi karibuni

Jeshi la Sudan limetangaza Alhamisi hii "kukaribia" kuundwa kwa serikali, siku kumi baada ya mapinduzi ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, yaliyolaaniwa na jumuiya ya kimataifa.

Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan Abdulrahman.
Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan Abdulrahman. AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw. Burhane, ambaye alitawala nchi hiyo tangu 2019 na kuangusha utawala wa rais wa zamani Omar al-Bashir, Oktoba 25 alivunja serikali, aliwakamata viongozi wa kiraia na kutangaza hali ya hatari nchini humo.

Tangu wakati huo, Sudan, iliyotumbukia katika mdororo wa kisiasa na kiuchumi, iko kati ya wanajeshi wenye msimamo na waandamanaji wanaopinga mapinduzi. Jumuiya ya kimataifa imekwa ikitoa wito wa mazungumzo na kurejeshwa kwa mamlaka ya kiraia.

"Kuundwa kwa serikali kunakaribia," amesema mshauri wa Bw. Burhane, Taher Abou Haga, aliyenukuliwa na televisheni ya serikali.

Baada ya mapinduzi, Wasudan waliingia mitaani kwa wingi katika maandamano yaliyokandamizwa na vikosi vya usalama, na kuua takriban watu 12 na kujeruhi mamia, kulingana na kamati ya madaktari inayounga mkono demokrasia.

Maandamano madogo yalifanyika tena Alhamisi mjini Khartoum yakitaka "mwisho wa utawala wa kijeshi".

Mnamo 2019, umoja mtakatifu wa watu na jeshi ulikomesha miaka thelathini ya udikteta. Raia na askari waliunda mamlaka yenye jukumu la kuongoza nchi kwenye uchaguzi.

Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu aliyeondolewa madarakani Abdallah Hamdok, akiwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi hayo, alitoa wito wa kurejeshwa kwa serikali yake. Kwa upande wao, wanadiplomasia, wafanyabiashara, wasomi na waandishi wa habari wanajaribu kupatanisha, lakini bila mafanikio makubwa kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.