Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Nchi kadhaa zatoa wito wa pamoja wa kurejeshwa kwa serikali ya kiraia

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi mbili zinazofikiriwa kuwa na ushawishi kwa jeshi la Sudan, zimeungana na Marekani na Uingereza siku ya Jumatano katika wito wa pamoja wa "kurejeshwa mara moja" kwa serikali ya kiraia iliyopinduliwa na jeshi huko Khartoum.

Waziri mkuu wa Sudan aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita Abdalla Hamdok anataka wafungwa waachiwe huru na taasisi za serikali kurejeshwa kabla ya kuanza mazungumzo ya aina yoyote.
Waziri mkuu wa Sudan aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita Abdalla Hamdok anataka wafungwa waachiwe huru na taasisi za serikali kurejeshwa kabla ya kuanza mazungumzo ya aina yoyote. - AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Tunatoa wito wa kurejeshwa kwa haraka na kikamilifu kwa serikali ya mpito inayoongozwa na raia," nchi hizo nne zimesema katika taarifa ya pamoja.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Sudan aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita anataka wafungwa waachiwe huru na taasisi za serikali kurejeshwa kabla ya kuanza mazungumzo ya aina yoyote.

Hayo yanajiri wakati Jeshi nchini Sudan bado linaendelea na majadiliano na waziri mkuu aliyeondolewa madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita.

Kulingana na duru zilizoko karibu kabisa na waziri mkuu huyo mazungumzo yanayoendelea sasa yanaangazia uwezekano wa kiongozi huyo kurejea kuiongoza serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.