Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Juhudi za kidiplomasia zaongezeka huku mapigano yakikaribia mji mkuu

Hali ya hatari ilitangazwa na uhuru kusitishwa, baada ya waasi wa TPLF kuchukuwa hatua za kimkakati huko kaskazini mwa nchi na hivyo kuwafungulia njia kuelekea mji mkuu wa Addis Ababa.

Mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. ©GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo sasa yamehamia Kusini, lakini pia Mashariki, kuelekea barabara kuu ya kimkakati inayounganisha Addis Ababa na Djibouti.

 

Jeshi la shirikisho linaonekana kuimarisha ngome yake kuu katika mji mkuu, ambapo wanajeshi wengi kutoka uwanja wa vita wameonekana katika siku za hivi karibuni. Lakini pia kwenye mji wa Debre Berhan, mji wa mwisho kwenye barabara inayoelekea Addis Ababa, na ambako waasi wa TPLF sasa wanasonga mbele.

Baada ya kuidhibi miji ya Dessie na Kombolcha Kaskazini mwa nchi, waasi wa TPLF  wanasema wameungana na waasi wa Jeshi la Ukombozi la Oromo, ambalo wameapa kumpindua Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Makao makuu ya vikosi vya TPLF yanadai kuwa wamesonga mbele zaidi kusini na sasa wanadhibiti eneo la Kemise, kilomita 325 kutoka mji mkuu.

Mapigano makali pia yanaripotiwa mashariki mwa nchi, kwa kupigania udhibiti wa barabara ya kimkakati inayounganisha Addis Ababa na Djibouti.

Wasiwasi nchini Kenya

Ni kutokana na hali hii tete ambapo Jeffrey Feltman, Mjumbe Maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika, aliwasili Addis Ababa asubuhi ya leo kwa ziara ya siku mbili. Lengo lake ni kutetea tena suluhisho la amani kwa mzozo huo na kujaribu kukomesha uhasama.

Wakati huo huo, nchi za Afrika Mashariki zina wasi wasi na hali inayoendelea nchini Ethiopia. Nairobi inatoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo huo kusitisha mapigano, kukomesha matamshi ambayo yanaweza "kuchochea raia kushiriki katika mapigano", na kupendelea mazungumzo.

Hotuba hii inatofautiana na hotuba ya Uhuru Kenyatta mwezi mmoja uliopita mjini Addis Ababa, wakati wa kuapishwa kwa serikali mpya ya Ethiopia. Uhuru Kenyatta alimhakikishia Abiy Ahmed anamuunga mkono, bila kutaja mzozo unaoendelea. Lakini tangu wakati huo, hali imekuwa mbaya zaidi, hadi siku ya Jumanne, mamlaka ya Ethiopia ilitoa wito kwa wakazi wa mji mkuu kujihami dhidi ya waasi wa TPLF.

Polisi ya Kenya pia imetangaza kuwa imeimarisha mipango yao katika mpaka wake na Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.